Mahakama moja nchini Misri
imewahukumu vifo viongozi kumi wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim
Brotherhood kwa kuchochea ghasia zilizosababisha vifo vya watu wawili
mwezi July.
Washtakiwa wengine 38 akiwemo kiongozi wa kundi hilo Mohammed Badie watapewa hukumu yao ifikiapo mwezi ujao.Raia hao walipatikana na hatia ya kuchochea uma na kuzuia msafara wa magari katika mji wa Qalyub kazkazini mwa mji wa Cairo.
Wamekuwa wakishiriki katika maandamano dhidi ya jeshi ambalo lilimpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Bwana Badie tayari amehukumiwa kunyongwa katika kesi nyengine.
No comments:
Post a Comment