TANGAZO


Friday, June 6, 2014

Ni uhalifu kuwanyanyasa wanawake Misri


wanawake wa Misri

Kwa mara ya kwanza Misri imepitisha sheria inayotaja unyanyasaji wa wanawake kuwa uhalifu.
Chini ya sheria hiyo wanaume watafungwa miaka 5 gerezani kwa kuwanyanyasa wanawake hadharani au faraghani.
Sheria hiyo imepitishwa kama hatua ya mwisho kuchukuliwa na rais anayeondoka wa Misri Adly Mansour.
'Unyanyasaji umezidi'
Watetesi wa haki za wanawake nchini Misri wamesema kuwa unyanyasaji wa wanawake umefikia viwango vya kuhuzunisha. Utafiti uliofanywa umeonesha kuwa karibu wanawake wote wa Misri wamewahi kupitia unyanyasaji wa aina fulani iwe ya matusi au hata ubakaji.
Utafiti huo umeonesha kuwa hata mavazi ya kufunika mwili wote yanayopendekezwa na sheria za kiislamu nchini humo, hazijawazuia wanaume hao kuwanyanyasa wanawake.
Na sasa inahofiwa kuwa mapinduzi waliofanya mwaka wa 2011 hayakuleta mabadiliko yoyote.
Wanawake wengi wamelalamika kuwa walinyanyaswa wakiwa katika maandamano katika midani ya Tahrir.
'Tatizo liko kwa itikadi mbovu'
Watetesi hao wa haki wanasema kuwa polisi mara nyingi wanawalaumu waathiriwa kuliko wale wanaofanya uhalifu huo.
Sasa sheria hii inachukuliwa kama hatua kubwa sana kusaidia tatizo hilo, ila hofu ni kwa utekelezaji wake. Wadadisi wanasema kuwa itakuwa vigumu zaidi kubadilisha itikadi za watu juu ya unyanuasaji wa wanawake nchini humo.

No comments:

Post a Comment