Kiongozi wa waisilamu katika jimbo la Kano nchini Ngeria,Al-Haji Ado Bayero, amefariki.
Kiongozi huyo mwenye kuheshimiwa sana miongoni mwa viongozi wengine wote nchini humo , amethibitishwa kufariki nchini humo.Tangu wakati huo Nigeria imekabiliana na misukosuko ya mapinduzi ya kijeshi na ghasia zingine.
Alikuwa na umri wa miaka 84 na kutambuliwa kama kiongozi wa muda mrefu sana na mkongwe zaidi wa waisilamu katika jimbo hilo na pia alitambulika kama kiongozi wa pili mwenye ushaiwishi zaidi kwa waisilamu Nigeria
Miaka miwili iliyopita alinusurika kwa tundu la sindano baada ya msafara wake kushambuliwa ambapo dereva wake na walinzi wake wawili walifariki.
Ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali, Boko Haram, ndio waliomshambulia.
Mwandishi wa BBC Sa'ad Abdullahi mjini Abuja anasema kuwa emiralikuwa amerejea tu kutoka mjini London ambako alikuwa anapokea matibabu.
Maishani mwake alikuwa mfanyakazi wa banki, polisi, mbunge , balozi na mfanyabiashara maarufu.
No comments:
Post a Comment