TANGAZO


Sunday, May 4, 2014

Waziri Mkuu wa Ukraine ayalaumu majeshi





Waziri mkuu wa Ukraine, Aserniy Yatsenyuk

Waziri mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk amevilaumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kuzuia ghasia kusini mwa mji wa Odessa zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 40 kuuawa.
Arseniy Yatsenyuk amesema: "Binafsi navilaumu vikosi vya usalama na polisi kwa kushindwa kuzuia msako huu."
Bwana Yatsenyuk ameiambia BBC kuwa "kutakuwa na uchunguzi kamili na wa kina".
Wengi wa waliouawa ni wale wanaounga mkono Urusi ambao walikufa kutokana na moto baada ya kujificha katika jengo moja.


Polisi wakiwa mbele ya jengo la Vyama vya Wafanyakazi huko Odessa
Kauli ya Waziri Mkuu imekuja wakati majeshi ya Ukraine yakiuzingira mji wa Sloviansk mashariki mwa Ukraine ambao ni ngome kuu ya watu wanaoiunga mkono Urusi.
Watu wapatao 42 waliuawa katika mji wa Odessa Ijumaa, wengi wao kutokana na moto katika jengo la Vyama vya Wafanyakazi, ambamo waandamanaji walijificha kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya wanaoiunga mkono Urusi na wanaharakati wanaoiunga mkono Ukraine.
Bwana Yatsenyuk ameyalaumu makundi ya wanaoiunga mkono Urusi kwa kusababisha ghasia.
Ameishutumu Urusi na waandamanaji wafuasi wake kwa kutangaza "vita kamili...kuitokomeza Ukraine na kutokomeza uhuru wa Ukraine".

No comments:

Post a Comment