Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Zanzibar Said Ali Mbarouk, akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, inayoadhimishwa May 3 ya kila Mwaka. Maadhimishi hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa SUZA Vuga Zanzibar. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews)
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ndg. Kajubi Mukajanga, akitowa maelezo ya historia ya Vyombo vya habari duniani kuazishwa kwake, na kuzungumzia Zanzibar ni Nchi ya kwanza katika afrika mashariki kuazisha kwa Vyombo vya habari.
Meneja Viwanja na Udhibiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bi. Pili Mtambalike, akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho hayo na kutoa maelezo ya majalada yanayotayarishwa na MCT, ili kuzinduliwa katika siku hii ya Uhuru Vyombo vya Habari Duniani katika ukumbi wa SUZA Vuga, mjini Zanzibar jana.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk, akikabidhiwa vitabu mbalimbali vilivyotayarisha na MCT katika utafiti wake kwa Vyombo vya Habari Tanzania. Jumla ya vitabu vinne vimezinduliwa katika maadhimisho hayo.
Waziri wa Habari UtamaduniUtalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, akizindua moja ya Vitambu vinne ambavyo vilizinduliwa katika maadhimisho hayo katika ukumbi wa SUZA Vuga. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Zanzibar Ndg. Rafii Haji na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ndg. Kajubi Mkukajanga, wakisuhudia uzinduzi huo.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said AliMbarouk, akionesha vitabu alivyovizinguwa mbele ya waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliofanyika Kitaifa Zanzibar..
Waandishi wa Habari wa Vyombombalimbali wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Habari alipokuwa akihutubia katika maadhimisho hayo ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Viongozi na Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho hayo ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA, Zanzibar.
Mwandishi wa habari Mkongwe Zanzibar Ndg. Enzi Talib, akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Waandishi wa Habari katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Meneja wa Baraza la Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Ndg. Suleiman Seif. akitowa utaratibu wa mkutano huo wa Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari , utaratibu wa maadhimisho hayo kwa Wageni waalikwa na Wanahabari wa Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia michezo iliopamba Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, katika ukumbin wa SUZA Vuga Zanzibar.
Msanii Othman Makombora akitowa burudani katika maadhimisho hayo kwa Kupiga upatu kuwahamasisha waandishi kuamka kufanya kazi zao za uandishi kwa jamii.
Wasanii wa Kikundi cha Kwerekwe wakicheza ngoma ya kibati.
Mratibu wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi za Zanzibar Bi. Shuffa Said akifurahii maadhimisho hayo kwa kucheza ngoma ya kibati.
Vikatuni wakitowa ujumbe katika maadhimisho hayo.
Msanii wa kusoma Utenzi bila ya kuandika katika karatasi Kassim Yussuf akisoma utenzi wa Siku ya Vyombo vya Habari.
Viongozi wa MCT wakiwa katika ukumbi wa hafla ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Mjumbe wa Tume ya Katiba Ndg. AliSaleh akitowa mada katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yenye kuzungumzia. Kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari, wa Kujieleza na Haki ya Kupata Habari ndani ya Katiba(The Constitution review process : Safeguarding Constitution Guarantees on Freedom of Expression and the press and Accessto Information)
Mtoa Mada Ndg. Atillio Tagalile, akitowa mada yake inayozungumzia Usalama wa Waandishi wa Habari Tanzania : Changamoto kwa Vyombo vya Dola kwa Kushindwa Kuchukua hatua dhidi ya Uonevu kwa Waandishi wa Habari na Utawala Sheria (Making Journalists Safe in Tanzania :Challenges of Impunity and the Rule of Law)
Dkt. Omar Dadi Shajak akitowa mada yake kwa Waandishi wa habari katika Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, inayozungumzia Media for Development Empowering Communities through Free Information Exchange and Knowledge Sharing.
No comments:
Post a Comment