TANGAZO


Sunday, May 4, 2014

Mkutano wa CCM Zanzibar wafana

* Wana UKAWA wachanwa chanwa waambiwa wana uroho wa madaraka wa kutaka Serikali Tatu 

* Wadaiwa kutaka kuuvunja Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar

Wananchi wakishangilia na kuonesha vidole kuunga mkono Serikali mbili za Muungano, wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar. Mkutano huo uliudhuriwa na viongozi mbalimbali  akiwemo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana. (Picha zote na Kamanda wa Matukio Blog)
Mama Fatma Karume akihutubia katika mkutano huo na kukemea Ukawa wanaotaka kuuvunja Muungano kwa kutaka Serikali Tatu katika mabadiliko ya Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhman Kinana akimpongeza Mjane wa Hayati Abeid Amani Karume, Mama Fatuma Karume kwa hotuba yake nzuri katika mkutano huo.
Wananchi wakishangilia katika mkutano huo, hasa baada ya Mjumbe wa NEC, Mohamed Seif Khatib kumuelezea Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuwa na tabia ya kinyonga  kuhusu suala la Muungano, ambapo awali alikuwa muumini Muungano wa Serikali tatu, mara wa mkataba na sasa anataka Serikali tatu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimpongeza Mohamed Seif Khatibu kwa hotuba yake nzuri.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Hamza Hassan Juma, akielezea kwenye mkutano huo, kuhusu mambo mbalimbali yaliyokubaliwa kuwekwa kwenye Katiba  Mpya ili kupunguza kero mbalimbali za Wazanzibari kwenye Muungano.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Steven Wassira akiwaeleza wana Ukawa kuwa hawawezi kutenganisha Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar kama ilivyo uhusiano wa Uhuru wa Tanganyika na Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Idd akihutubia katika mkutano huo na kupendekeza UKAWA kufutwa kwa vile haina uhalali wowote akidai kuwa si Chama kwani haina usajili. Alisema kuwa Ukawa imeundwa kwa lengo la kuuvunja Muungano uliodumu kwa miaka 50 na kudumisha amani na umoja kwa Tanzania.
Kinana akihutubia katika mkutano huo na kutamka kuwa CCM itasimama kidete kuhakikiasha uchumi wa Zanzibar unaimarika.
 Kinana na viongozi wengine wakiuombea dua Muungano wa Tanzania pamoja viongozi waanzilishi wa muungano huo, ambao ni Julius Nyerere na Abeid Karume.
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akikemea kitendo cha viongozi wa UKAWA kungea uongo na tabia ya kuwakejeli waasisi wa Muungano wa Tanzania.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Asha Bakari Makame akimchana chana Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kwa tabia yake ya kinyonga kuhusu muundo wa Muungano.

 Mamboo poa.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ummy Mwalimu akielezea jambo kuhusu mwenendo usiofaa wa UKAWA  kukimbia vikao vya bunge hilo. 
Mjumbe wa Bunge la Katiba Emmanuel Nchimbi akinukuuu kwenye kitabu kilichotungwa na Maalim Seif Sharif Hamad kinachopinga Muungano.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo ambapo alipingana na viongozo wanaowabebembeleza wananchama wa Ukawa kurudi katika Bunge la Katiba, akidai waachwe kwani tangu walipoondoka bunge limekuwa la kistaraabu.

No comments:

Post a Comment