TANGAZO


Thursday, May 22, 2014

Urusi yaudhiwa na kauli ya Prince Charles






Priince Charles na mkewe Camilla wakiwa katika ziara yao nchini Canada

Naibu balozi wa Urusi mjini London ameomba kukutana na maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa Uingereza kujadili matamshi ya Mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles ambapo amefananisha vitendo vya Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Ukraine na uliokuwa utawala wa kinazi nchini Ujerumani chini ya Adolf Hitler.
Prince Charles ambaye yuko kwenye foleni kumrithi Malkia wa Uingereza, alitoa matamshi yake Jumatano alipokuwa anazungumza na mfanyakazi mmoja wa Poland katika makavazi ya wahamiaji eneo la Nova Scotia.
Walikuwa wanajadili hatua ya Hitler kunyakua nchi wakati wa utawala wake wakati ambapo mwanamfalme huyo alipofananisha kitendo hicho na kilichofanyika nchini Ukraine kwa maagizo ya Rais Vladimnir Puti.
Prince Charles anatarajiwa kuhudhuria hafla moja nchini Ufaransa mwaka ujao.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, amesema kuwa sio jambo la kawaida mwanamfalme kutoa kauli za kisiasa wakati wa mzungumzo ya faragha na kwamba kwa sasa hawawezi kutamka lolote kuhusu zogo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu, Prince Charles na mkewe Camilla walitembelea makavazi ya kitaifa ya wahamiaji nchini Canada, wakati wa ziara yao ya siku nne nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema kuwa ombi la kufanyika mkutano ni dalili ya Urusi kukasirishwa na matamshi ya Prince Charles ingawa Urusi imejizuia kugeuza swala hilo na kulifanya kuwa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
Inaaminika kuwa Urusi inataka ufafanuzi kuhusu matamshi ya Mwanamfalme huyo.

No comments:

Post a Comment