TANGAZO


Thursday, May 22, 2014

Barua pepe zatumiwa kujumlisha kura Malawi




Wagombea katika uchaguzi wa Malawi
Maafisa wa uchaguzi nchini Malawi, wanasema kuwa wamelazimika kutumia vipepesi na barua pepe kujumlisha kura za uchaguzi mkuu baada ya mfumo wa elektroniki kuharibika.
Makarani wa tume ya uchaguzi waliopo mashinani wameshindwa kutuma tarakimu za matokeo ya kura hizo.
Haya ndio matatizo ya hivi punde kushuhudiwa katika uchaguzi huo lakini maafisa wamesema wamejitolea kufanya kazi.


Shughuli ya kupiga kura iliongezwa muda kwa siku ya pili
Katika baadhi ya maeneo masanduku ya kura hayakuwasilishwa na baadhi ya vituo vilifunguliwa kuchelewa siku ya jumanne na kulazimisha maafisa kutumia ndoo na katarasi za plastiki kukusanya kura.
Raia wa sasa Joyce Banda anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wengine kumi na moja.
Baadhi ya vituo vilifungua kuchelewa Jumanne na kusababisha shughuli ya upigaji kura kuongezwa muda kwa siku ya pili.
Rais wa sasa Joyce Banda,anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wengine 11.

No comments:

Post a Comment