*Asema Serikali ya Tanzania ipo imara katika kuendelea na kusimamia juhudi zinazofanywa na Banki ya Afrika
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum, akiwa katika majadiliano na viongozi wa
Benki ya HSBC kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
‘Terminal III’. Majadiliano hayo, yalifanyika katika Hotel ya Mills
Colonie Mjini Kigali Rwanda.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada
Mkuya Salum, akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya HSBC,
baada ya majadiliano yaliyofanyika katika Hotel ya Mills Colonie Kigali
nchini Rwanda.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum, akimsikiliza Bi. Erika Rubin, Mratibu wa mfuko wa Mkoba Fund, wakati wa mkutano wao, uliofanyika katika
Hotel ya Serena, Mjini Kigali Rwanda. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Ndg. Jovin
Rugemarila, Afisa anayeshughulikia masuala ya ADB na mbele yake ni
Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje – Wizara ya Fedha Ndg. Jarome Bureta.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada
Salum Mkuya, akiwa kwenye mazungumzo ya faragha na Mratibu wa Mkoba Fund,
Bi. Erika Rubin mara baada ya mkutano wao, uliofanyika katika ukumbi wa
Muhabura, Mjini Kigali Rwanda.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedhda, Dkt. Silvacius Likwilile akieleza kwa muhtasari
yale yaliyojadiliwa katika mikutano ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB),
inayoendelea nchini Rwanda. Anayemhoji ni mtangazaji wa TBC ndg. Stanley Ganzel.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada M. Salum akifafanua jambo katika moja ya Mikutano ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na watendaji wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasimali Tanzania (TIB), Bw. Peter Noni.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofunguliwa na Mhe. Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini Kigali Rwanda.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada M. Salum akifafanua jambo katika moja ya Mikutano ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na watendaji wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasimali Tanzania (TIB), Bw. Peter Noni.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofunguliwa na Mhe. Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini Kigali Rwanda.
Na Mwandishi wetu, Kigali, Rwanda, 22/5/2014
SERIKALI ya Tanzania ipo imara katika kuendelea na kusimamia
juhudi zinazofanywa na Banki ya Afrika katika kuinua mitaji kupitia mpango wa
sita wa kukuza mitaji wa benki hiyo (GCI-VI).
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum leo, alipokuwa akitoa hotuba yake kwa Magavana wa nchi za
Afrika katika mkutano wa mwaka wa wadau wa Benki ya Afrika jijini Kigali, Rwanda.
Mh. Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa na uwezo wa kulipa hisa zake
zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda
uliopangwa.
Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI
Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kulipa hisa zake zipatazo Dola za
Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Zaidi ya hayo, Waziri Saada
ameendelea kusema kuwa nchi yake imeweza kulipa hisa zake za awamu ya nne
zipatazo kiasi cha Dola za Kimareka 1,279.30 kabala ya muda uliopangwa.
“Ninaamini ni katika mkutano huu
tunaweza kujadili dira ya Benki katika miaka mingine 50 ijayo kama kauli mbiu
ya mkutano huu inavyothibitisha, “Afrika tunayoitaka miaka 50 ijayo” alisema
Waziri Saada.
Aidha, Waziri Saada alimpongeza
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Donald Kaberuka na uongozi mzima kwa kusimamia
na kuongoza kwa umahiri mkubwa majukumu walionayo ya kibenki na kuhakikisha
inasonga mbele daima na kuifanya kuwa benki bora barani humu.
Ili kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa bara hili lazima
kudumisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kijamii na kujipatia
maendeleo endelevu kwa nchi zao na watu wake. Mwaka
huu Benki ya Afrika inafikisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake ambapo imeendelea
kuhudumia bara hili kwa mafanikio makubwa.
Kwa upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame akifungua mkutano
huo alisema kuwa ili kufikia uchumi wa kati katika Bara la Afrika kwa miaka 50 ijayo inabidi nguvu kubwa ielekezwe kwenye
sekta binafsi ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na wanawake.
Mkutano huo ni wa siku
tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu ambapo kabla ya ufunguzi wa Mkutano huu
ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana ambao ni Mawaziri wa Fedha
kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiambatana na wajumbe kuwakilisha nchi
zao.
No comments:
Post a Comment