Watu wanaokadiriwa kufikia sita wakufa kutokana na mlipuko mkubwa wa bomu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mwandishi wa habari wa BBC katika mji huo
anasema watu sita akiwemo kiongozi wa zamani wa serikali ya mtaa ni
miongoni mwa waliokufa.Mlipuko huo uliotokea karibu na katikati mwa mji umesabbaishwa na bomu lililotegwa kandokando ya barabara.
Mashambulizi mengi yamekuwa yakitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al Shaabab, ambalo linakabiliana na operesheni kubwa kutoka kwa vikosi vya umoja wa Afrika AMISOM kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia.
Kundi hilo limejiondoa kwenye miji mingi lakini bado lina nguvu linashikilia miji kwenye maeneo ya vijijini ya Kusini na Katikati mwa Somalia.
No comments:
Post a Comment