TANGAZO


Monday, May 26, 2014

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AfDB wamalizika jijini Kigali


Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki ndg. Gabriel Negatu katika mkutano uliofanyika katika ukumb wa Ecobank jijini Kigali, Rwanda. 

Mhe.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akijadiliana jambo na mmoja wa washiriki wa Mkutano wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unafanyika Kigali Rwanda. Pembeni ni mwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile na Msaidizi wa Waziri, Bw. Thomas Mabeba.



Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkuatno mkuu wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika uliofanyika Kigali nchini Rwanda.




Na Mwandish wetu- Kigali, Rwanda

VIONGOZI wa Benki Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wameahidi kuijenga Afrika itakayoendelea kuwa na umoja, mshikamano na yenye miundombinu ya uhakika. 

Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Benki ya AfDB, Dkt. Donald Kaberuka alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa 49 wa banki hiyo jijini Kigali, Rwanda. Rais wa Benki hiyo, Dkt. Kaberuka alisema Benki itasaidia utekelezaji wa mipango bora ambayo itatokana na majadiliano yatakayofikiwa kwenye vikao nchi wananchama.



Miongoni mwa vipaumbele vya benki kwa kipindi cha miaka kumi ijayo ni kujenga mazingira ya kuwa na uchumi imara na endelevu, usimamizi wa maliasili za bara la Afrika na ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha zaidi wanawake na vijana katika ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika. Katika kuhakikisha maendeleo ya Bara la Afrika yanafikiwa kupitia Benki ya AfDB kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni  pamoja na kusimamia utekelezaji wa mpango wa ‘Afrika 50’ ambao utapelekea kuongeza ufadhili wa kiasi cha Dola bilioni 100 ambazo zinahitajika katika kuimarisha miundombinu ya Bara la Afrika.



Awali katika mkutano uliofanyika kati ya Mkurugenzi wa AfDB kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu na ujumbe wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa jitihada zake za kuhakikisha Tanzania inatekeleza kwa ufanisi miradi yote inayofadhiliwa na Benki hiyo.“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambayo inanufaika na fedha kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika,kwa sasa tuna zaidi ya miradi 31 ambayo inatekelezwa na AfDB”  alisema Dkt. Likwilile.



Mwishoni mwa Mkutano wa Magavana wa Benki, Pia walipitisha kuanzishwa kwa Mfuko wa Pamoja wa Ukuaji wa Afrika (AGTF) na kiasi cha dola bilioni 2 zitatolewa na China ili kuwezesha AfDB kukabiliana na kuongezeka kwa mahitaji ya kikanda kwa nchi wanachama wa benki na wateja wa sekta binafsi.



Mkutano ujao wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika utafanyika Jijini Abidjan,nchini Ivory Coast ambayo pia itakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki ya maendeleo ya Afrika yatakayoadhimishwa Novemba, 2015.

No comments:

Post a Comment