TANGAZO


Monday, May 26, 2014

Rais Kikwete ahudhuria sherehe za kuapishwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini jana, Mei 24, 2014.
Rais Jacob Zuma akila kiapo katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria wakati wa sherehe za kuapishwa kwake jana, Mei 24, 2014. 

Ndege za kijeshi zikiunda umbo la "20" kuashiria kutimia miaka ishirini ya uhuru kamili wa Afrika Kusini katika sherehe za kuapa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini jana, Mei 24, 2014.


Marais na viongozi toka nchi mbalimbali wakiondoka, baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment