TANGAZO


Monday, May 26, 2014

CCM wafunika mkutano wa Singida Mjini

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Peoples, Mjini Singida jana, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya chama hicho, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Sehemu ya umati katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Singida jana.
Wananchi wakishangilia wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba wakiwapungia mikono wananchi walipowasili jana katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Peoples, Mjini Singida, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akionesha ishara ya chama hicho, wakati wa msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ulioongozwa kwa pikipiki na bajaji kuelekea katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Peoples, Mjini Singida. Kushoto kwake ni Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji. Kinana yupo mkoani Singida kwa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana, Nape na Nchemba wakiwapungia mikono wananchi walipowasili kwenye mkutano huo.
Kinana akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali ziliziokuwa zikioneshwa kwenye mkutano huo.
Kikundi cha wajasiriamali wauza mbogamboga na matunda nao wahakukosa katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira, wakati wa mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji akitaja utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kwa asilimia kubwa ameifadhili katika jimbo hilo.
Katibu Mkuu Kinana (katikati), akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji (kushoto), pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, wakati wa mkutano huo, wa hadhara.
Katibu Kinana akikabidhi msaada wa saruji kwa moja ya vikundi vya wajasiriamali vilivyofadhiliwa na Dewji.
Sehemu ya umati wa wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu Kinana akihutubia katika mkutano huo.
Mbunge Dewji (kushoto), akiwa na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika mkutano huo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu Kinana (wa tatu kulia), akitembelea Hospitali ya Rufaa ya Singida jana.
Katibu Kinana akipata maelezo kuhusu vifaa vya upasuaji katika hospitali hiyo.
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Singida, alipotembelea kituo cha usambazaji maji Singida Mjini.

No comments:

Post a Comment