TANGAZO


Thursday, May 29, 2014

Matukio mbalimbali katika Bunge la Bajeti leo

Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba (kushoto) na Assumpter Mshama wakiingia bungeni mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Naibu wake, George Simbachawene (katikati mbele), wakiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Wilaya ya Muleba mkoani Bukoba waliofika bungeni mjini Dodoma jana, kusikiliza hotuba ya wizara hiyo kwa mualiko wa Waziri Tibaijuka.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitafakari jambo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (kulia), akiteta jambo na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye ni Mbunge wa Hai, Freeman Man Mbowe (kulia), akisalimiana na wageni wake wa jamii ya kimasai walipotembelea bungeni mjini Dodoma jana. Wa pili kulia ni Mbunge wa Tabora mjini, Aden Rage. (Picha zote na Dotto Mwaibale)

No comments:

Post a Comment