TANGAZO


Thursday, May 29, 2014

Safari ya mwisho ya marehemu Maxmilian Ngobe

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mpiga picha wa Kituo cha Telesheni cha Mlimani Tv, marehemu Maxmilian John Ngube (Papa Max), likiwa kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam jana mchana tayari kwa kuagwa na kisha kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni jijini. Marehemu Max Ngobe alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na maradhi ya moyo, yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Risala fupi ikisomwa wakati wa Shughuli hiyo na Kuangwa kwa Marehemu Max Ngobe mmoja wa wanahabari wakongwe Tanzania.
Wanahabari wakirekodi tukio la kuaga Mwili wa Marehemu Max.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuaga mwili wa Marehemu Max.

No comments:

Post a Comment