Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Serikali na Mashirika ya Umma katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, ambapo siku hii kila mwaka huadhimishwa. Sherehe hizo zimefanyika leo katika Viwanja vya Salama Bwawani, Mjini Unguja. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Wafanyakazi wa Benki ya Tanzania (BOT) ni miongoni mwa wafanyakazi walioshiriki katika maandamano ya siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bandari wakimsalimia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipkuwa akipokea maandamano ya wafanyakazi katika kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani Meimosi leo katika viwanja vya Salama Bwawani, Mjini Unguja.
Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya walijumuika katika maandamanio ya wafanyakazi mbali mbali katika kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo asubuhi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya viongozi na Wafanyakazi wa idara mbalimbali za Serikali na mashirika ya Umma, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipkuwa akitoa hutuba yake wakati wa kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani Meimosi leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akishikana mikono na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZATUC Taifa Zahran Mohammed Nassor (kulia) na Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma,ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri, kama ni ishara ya mshikamano wakati wa kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Waziri Ismal Waziri,kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,chama cha ZUPHE,akiwa ni miongoni wafanyakazi bora waliopewa zawadi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani,zilizofayika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Fatma Juma Ramadhan, chama cha Chodawu,akiwa ni miongoni wafanyakazi bora waliopewa zawadi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani, zilizofayika leo, katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
No comments:
Post a Comment