Maelfu ya wanariadha wanatarajiwa kushiriki mbio za Boston Marathon baadaye hii leo huku kukiwa na usalama wa hali ya juu.
Mbio hizo za kila mwaka zinafanyika baada ya mlipuko wa bomu kuwaua watu watatu na kuwajeruhi mamia wengine wakati wa mbio hizo mwaka jana.
Mashabiki nao pia watakaguliwa na wataruhusiwa kubeba tu mifuko ya plastiki inayoonyesha vitu walivyobeba.Makundi ya Polisi kutoka majimbo mengi pamoja na wale waliovaa sare za raia wamepelekwa katika mkondo wa mbio hizo kuimarisha usalama.
Wanariadha elfu 36 watashiriki katika mbio hizo zaidi ya idadi ya kawaida iliyotarajiwa.
Wanariadha watakaa kimya kwa sekunde kadhaa katika mwanzo wa mbio hizo ili kuwakumbuka waathiriwa wa mkasa wa bomu.
No comments:
Post a Comment