Watu milioni 814 watachagua kati ya chama kinachotawala cha Congress na chama cha Upinzani cha Hindu nationalist BJP .
Uchaguzi huu utaandaliwa katika mikondo 9 zikianzia majimbo ya Assam na Tripura zilizoko Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo kubwa.
Shughuli hiyo kubwa zaidi ya Kidemokrasia duniani itachukua majuma matano kukamilika kutokana na changamoto ya maswala ya mipango usalama na idadi .
Chama kinachotawala cha Congress kinakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa chama cha mrengo wa kulia cha Hindu BJP, kinachoongozwa na Narendra Hodi, kiongozi mbishi mwenye ushawishi mkubwa kutoka Magharibi mwa Gujerati.
Kampeni za uchaguzi huo zimetawaliwa na maswala ya ufisadi pamoja na mfumuko wa bei ya bidhaa za Chakula.
Uchaguzi India
7 April - 2 Majimbo 6 Maeneo Bunge
9 April - 5 Majimbo 7 Maeneo Bunge
10 April - 14 Majimbo 92 Maeneo Bunge
12 April - 3 Majimbo 5 Maeneo Bunge
17 April - 13 Majimbo 142 Maeneo Bunge
24 April - 12 Majimbo 117 Maeneo Bunge
30 April - 9 Majimbo 89 Maeneo Bunge
7 May - 7 Majimbo 64 Maeneo Bunge
12 May - 3 Majimbo 41 Maeneo Bunge
6 May - Kuhesabiwa kwa Kura
9 April - 5 Majimbo 7 Maeneo Bunge
10 April - 14 Majimbo 92 Maeneo Bunge
12 April - 3 Majimbo 5 Maeneo Bunge
17 April - 13 Majimbo 142 Maeneo Bunge
24 April - 12 Majimbo 117 Maeneo Bunge
30 April - 9 Majimbo 89 Maeneo Bunge
7 May - 7 Majimbo 64 Maeneo Bunge
12 May - 3 Majimbo 41 Maeneo Bunge
6 May - Kuhesabiwa kwa Kura
Chama hicho kipya kiliwaduwaza wachanganuzi wa maswala ya kisiasa nchini humo kilipotwaa ushindi muhimu katika Uchaguzi mdogo uliofanyika mji mkuu wa India New Delhi mwaka uliopita.
Chama hicho sasa kimewakilisha wagombea katika maeneo bunge yote 543
Bunge la chini la kitaifa ( Lok Sabha) linawajumbe 543 na chama chochote kinahitaji ushindi wa wajumbe 272 kuunda serikali mpya .
Kutakuwa na vituo 930,000 takriban vituo laki moja zaidi ya vituo vilivyotumika mwaka wa 2009.
Mashini za kielektroniki za kupigia kura zitatumika na kwa mara ya kwanza hazitajumuisha kidude cha kutowachagua wawakilishi waliosajiliwa yaani None of the Above (Nota).
Mwandishi wa BBC aliyeko katika jimbo la Assam, Sanjoy Majumderameripoti kuwa wapiga kura walijitokeza kwa wingi asubuhi na mapema wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya Sari huku wakiwa
wamejitanda mitandio ya Kiassamese.
Wagombea wakuu ni mwakilishi wa familia ya Nehru-Gandhi, Rahul Gandhi wa chama cha Congress ambaye atakuwa akipambana dhidi ya Narendra Modi wa chama kikubwa cha upinzani BJP.
No comments:
Post a Comment