TANGAZO


Sunday, April 6, 2014

Matukio mbalimbali ya Bunge Maalum la Katiba wiki hii

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Andrew Chenge (katikati), Richard Ndassa (kushoto) na William Ngeleja (kulia), wakibadlishana mawazo mjini Dodoma juzi, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (kulia), wakibadilishana mawazo mjini Dodoma juzi na Mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Sophia Simba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (kushoto), wakibadilishana mawazo juzi, mjini Dodoma na Mjumbe wa Bunge hilo, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kushoto) akisalimiana na watoto waliofika Bungeni juzi kwa ajili ya kujifunza uendeshaji wa Bunge.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(kulia) akibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mjini Dodoma na Mjumbe mwenzie Donald Mtetemela (kushoto) mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anna Abdallah (kushoto), akiwaeleza jambo wajumbe wenzake, Askofu Donald Mtetemelwa (katikati) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, kwenye viwanja vya Bunge mara baada ya kuaghirishwa kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma juzi.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dk. Emmanuel Makaida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) mjini Dodoma juzi, kuhusu nia yake ya kulishitaki gazeti moja kwa kumwandika kuwa amemteua mke wake kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba.
Baadhi wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge, tayari kwa ajili ya kuendelea na vikao vya bunge hilo, mjini Dodoma juzi.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia (kushoto) na Mjumbe mwenziwe Rosemary Kirigini, wakiwasili bungeni kwa ajili ya kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma juzi kwa ajili kikao cha asubuhi.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika akichangia azimio la kufanyia marekebisho Kanuni za bunge hilo, juzi mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Moses Machari, akichangia azimio la kufanyia marekebisho Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma juzi.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto), wakibadilishana mawazo juzi, mjini Dodoma na Mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Stephen Wassira.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto), walipokuwa wakibadilishana mawazo juzi, mjini Dodoma na Mjumbe wa Bunge hilo, Salehe Pamba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Felix Mkosamali  akichangia hoja ya kufanyia marekebisho Kanuni za bunge hilo, ambapo aliunga mkono azimio hilo mjini Dodoma juzi.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Seleman Jafo, akichangia azimio la kufanyia marekebisho Kanuni za bunge hilo juzi, mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akichangia na kuunga mkono azimio la kufanyia marekebisho ya kanuni za bunge hilo, juzi mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan akiendesha kikao cha bunge hilo, kilichokuwa kikifanyia marekebisho Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma juzi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akiwasilisha marekebisho ya kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma juzi.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan akiondoka ukumbini mara baada ya kuaghirisha kikao cha bunge hilo, Maalum la Katiba kilichofanyia marekebisho Kanuni zake, mjini Dodoma juzi.
Mwenyekiti wa Kamati namba sita (6), ya Bunge Maaalum la Katiba, Stephen Wassira, akiongea na waandishi wa habari, mjini Dodoma juzi kuhusu mambo yaliyojitokeza katika Kamati yake hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati namba tano (5), Hamad Rashid Mohamed, akiongea na waandishi wa habari, mjini Dodoma juzi kuhusu mambo yaliyojitokeza katika Kamati yake hiyo, wakati wa majadiliano kwa Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akiongea na waandishi wa habari, mjini Dodoma juzi, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Afya duniani, April 7, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Mng’ato mmoja madhara Makubwa. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya. (Picha zote na kamati ya Bunge Maalum la Katiba)

No comments:

Post a Comment