TANGAZO


Tuesday, April 1, 2014

Japan yaisaidia Tanzania katika sekta ya kilimo

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), akitia saini hati ya makubaliano ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6, unaolenga kukuza sekta ya kilimo uliotolewa  na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okanda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), akibadilishana nakala ya makubaliano waliosaini na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okanda (kulia), ambayo yanahusu msaada uliotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la misaada ya Kimaendeleo la Japan (JAICA) leo, jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini, Yasunori Onishi akibadilishana nakala za mkataba waliosaini na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okanda (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo, jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Japan nchini, Masaki Okanda (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mkataba na Serikali ya Japan leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi).

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) . 

Kauli hiyo, ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada huo,  ambao utatumika katika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini nchini. 

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo, utatumika kununulia mbolea (UREA), ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo wadogo nchini ili kuongeza kipato chao.

Katibu Mkuu huyo, alisema kuwa msaada huo, umekuja muda muafaka ambapo Serikali inachukua hutua za makusudi katika kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri Watanzania takribani asilimia 74 nchini.  

Aidha, Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo na kumhakikishia Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okanda kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA, utatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake  Balozi wa Japan nchini, Masaki Okanda alisema kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia shirika la JAICA, unalenga zaidi kukuza sekta ya kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo. 

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini, Yasunori Onishi alisema kuwa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria, ulianzishwa tangu mwakqa 1974, ambapo Mkoa wa Kilimanjaro, ulikuwa unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.

Akimshukuru Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini  Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Yamungu Kayandabila, alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini. 

Serikali ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamia kilimo inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na hivyo kupunguza umasikini nchini.

No comments:

Post a Comment