Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya chama hicho, Ridhwani Kikwete, wakati wa kufunga kampeni jimboni Chalinze leo.(Picha zote na Othman Michuzi)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhwani Kikwete, akiwapungia wananchi wa jimbo hilo, wakati alipofika kwa ajili ya mkutano wa kufunga kampeni jimboni humo leo.Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akibadilishana mawazo na Mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa kufunga Kampeni leo,April 5,2014 kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze. Umati mkubwa wa wananchi wa Kijiji cha Kikaro, Kata ya Miono Jimbo la Chalinze wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro, Miono jimboni Chalinze,leo April 5,2014 tayari kwa kufunga kampeni za CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa kufunga Kampeni za chama hicho zilizofanyika leo April 5,2014 Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro, Miono jimboni Chalinze.
No comments:
Post a Comment