TANGAZO


Wednesday, April 30, 2014

BFT yampongeza Waziri Membe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

HIRIKISHO la ngimi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Waziri  wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Bernard Membe kwa hatua na jitihada alizozifanya  za kutafua na kufanikisha  kambi ya mazoezi kwa Timu ya Taifa ya ngumi  inayojiandaa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini Scotland.
Kwa hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na maandalizi ya Timu  yetu ya Taifa kwa kuitafatia  kambi ya mazoezi ya kimataifa Nchini Uturuki na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika hali duni  bila ya kuwa na vifaa vya kisasa kulingana na mabadiliko ya mchezo wa ngumi duniani.

Kwa kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri ya ushiriki waTanzania katika mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa mara ya kwanza Tanzania ilishiriki mwaka 1972 na Tanzania  kupata medali ya kwanza ya kimataifa baada ya   Tanzania kupata  uhuru, iliyoletwa na Bondia (LYTUS SIMBA) na baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta medali ni kama wafuatao:

MICHAEL YOMBAYOMBA   :  (Dhahabu)
HAJI  MATUMLA                     :   (Fedha)
MAKOYE ISANGURA             :   (Shaba)
MWAMBEYA   BAKARI        :   (Shaba)
WILLY  ISSANGURA              :   (Shaba)
LUCAS MSOMBA                   :   (Shaba)

Bado BFT tunamuomba azidi kutusaidia  vifaa zaidi hasa ulingo wa kisasa na Computer inayotumika  kuhesabia point za ushindi wakati wa mashindano kwani Nchi zote duniani ndizo wanazozitumia na niagizo kutoka chama cha ngumi cha dunia kwa wanachama wote lazima waitumie katika mashindano..

Taarifa hii imeletwa kwenu na                                
Makore Mashaga

KATIBU MKUU.

No comments:

Post a Comment