TANGAZO


Friday, March 14, 2014

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba waanza kula kiapo Bungeni leo, mjini Dodoma

 *Mwenyekiti, Makamu wake nao waapa kutumikia kazi zao kwa uaminifu



Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta akila kiapo mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad (kulia mbele), wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo, mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu wa bunge Hilo, Dk. Thomas Kashilila. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
 
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk. Thomas Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo, mjini Dodoma. Kulia ni Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad (mbele yake).
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akitoa hoja ya kutengua kifungu kwa ajili ya kuongeza muda wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo, mjini Dodoma.
 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta (kushoto), akimwapisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho (kulia), wakati wa kuwaapisha wajumbe wa bunge hilo, mjini Dodoma leo.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta (kushoto), akimwapisha mjumbe wa bunge hilo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), wakati wa kuwaapisha wajumbe wa bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa mjumbe wa bunge hilo, mbele ya Mwenyekiti, Samwel Sitta (kushoto), mjini Dodoma leo.
 
 
 

No comments:

Post a Comment