TANGAZO


Wednesday, March 12, 2014

Wahadhiri wa Vyuo vya umma wagoma Kenya


Wahadhiri wanadai kulipwa nyongeza ya mishahara
Mafunzo katika vyuo vikuu vya umma nchini Kenya yameathirika baada ya wahadhiri wa vyuo kuanza rasmi mgomo wa kitaifa.
Wahadhiri hao wamekiuka agizo la mahakama na kutogoma na kuamua kugoma.
Mgomo huo unajiri wakati serikali ya Kenya imewataka wafanyikazi wa serikali kukubali mishahara yao kupunguzwa hasa baada ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto pamoja na baraza la mawaziri kupunguza mishahara yao kutokana nagharama kubwa ya matumizi ya serikali.Wanailaumu serikali kwa kutotekeleza makubaliano ya nyongeza ya marupurupu yao kama ilivyoahidi mwaka jana.
Zaidi ya wafanyakazi 30,000 wa vyo vikuu wameanza kususia kazi baada ya waziri wa elimu kukosa kufikia makubaliano ya kusitisha mgomo huo ambapo wahadhri wanadai shilingi bilioni 3.9 kati ya wahadhiri na wakuu wa vyuo hivyo.
Kwa sasa idadi ya wanafunzi ambao watakosa mafunzo ni kati ya 200,000 na 300,000, ikiwa serikali haitaleta suluhu.
Mkutano wa awali kati ya waziri wa elimu na makatibu wake wawili, haukuzaa matunda.
Kiini cha mgogoro huo ni malipo ya awamu ya pili ya shilingi bilioni 7.8 ya nyongeza ya mishahara ambayo iliafikiwa mwaka 2012.
Pesa hizo zilipaswa kulipwa kwa awamu, huku nusu ya pesa hizo zikilipwa Disemba mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment