* Watakiwa kujenga hoja zenye nguvu kwa masuala ya wanawake na kuzitetea kwa sauti moja kwenye kamati zao za Bunge
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Anna Abdallah, akifafanua jambo wakati alipokuwa akiifungua semina ya Viongozi wa Azaki na Wabunge Wanawake katika kujenga muafaka wa agenda muhimu kwa masuala ya kijinsia, katika ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma leo. Kulia ni Makamu wake, Suzan Lyimo na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa TWPG, Dk. Mary Mwanjelwa. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Anna Abdallah, akifafanua jambo, mara baada ya kuifungua semina ya viongozi wa Azaki na Wabunge wanawake, mjini Dodoma leo. Wanasemina, wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TPWG), ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakisikiliza na kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Wanasemina, wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TPWG), ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakisikiliza na kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa TWPG, Suzan Lyimo akiwasilisha mada kuhusu Uwakilishi wa Wanawake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Wanasemina, wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TPWG), ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakisikiliza na kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Muelimishaji kutoka Mtandano wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya akiwasilisha mada kuhusu Haki za wanawake, Utu na hali ya maisha na mgawanyo wa rasilimali, katika semina hiyo.
Wanasemina, wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TPWG), ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakisikiliza na kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Muelimishaji kutoka kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Victoria Mandari akiwasilisha mada kuhusu Masuala ya Mirathi na Ndoa kwenye semina hiyo.
Mwanachama wa TWPG na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akitoa rai yake wakati akichangia kwenye semina hiyo, mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Anna Abdallah, akifafanua jambo katika semina hiyo ya viongozi wa Azaki na Wabunge wanawake katika kujenga muafaka wa agenda muhimu kwa masuala ya kijinsia. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa (TWPG), Dk. Mary Mwanjelwa.
Mwanachama wa TWPG na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anna Kilango, akichangia moja ya mada zilizowasilishwa katika semina hiyo.Mwanachama wa TWPG na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Panya Ali Abdallah, akizungumza na wanasemina hao, wakati alipokuwa akiifunga semina hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Anna Abdallah, akiwa na Makamu Mwenyekiti wake, Suzan Lyimo (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa (TWPG), Dk. Mary Mwanjelwa, wakiomba kwa Mungu, wakati wa kufungwa semina hiyo.
Wanasemina, wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TPWG), ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakiomba kwa Mungu, wakati wa kufungwa semina hiyo.Wanasemina, wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake Tanzania (TPWG), ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, pamoja na waelimishaji, wakiomba kwa Mungu, wakati wa kufungwa semina hiyo.
Mwanachama wa TWPG na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zainab Gama (kushoto), akijadili jambo na wanachama wenzake pamoja na watoa mada (Victoria Mandari (wa pili kulia) na Usu Mallya (wa pili kushoto), mara baada ya kufungwa semina hiyo.
Na Magreth Kinabo –MAELEZO, Dodoma.
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ametoa changamoto kwa wajumbe wenzake wanawake walio kwenye Bunge hilo, kujenga hoja zenye nguvu zinazohusu masuala yanayohusu wanawake na kuzitetea kwa sauti moja ili ziweze kupita katika Rasimu ya Katiba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe. Anne ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akitoa mchango wake kwa wajumbe wa semina ya kujenga agenda muhimu kwa masuala ya kijinsia iliyoandaliwa na Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (TWPG) kwa wajumbe wanawake wa Bunge hilo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa.
“ Ninawaomba tuwe na hoja zenye nguvu wakati wakuchangia mjdala wa Rasimu ya Katiba . Tukisimama kwa hoja za nguvu na kutetea vifungu vinavyohusu masuala ya wanawake tunaweza kubadilisha vifungu.
Tuzungumzeni hoja tuache kufanya fujo, tusiingie katika malumbano ambayo hayana tija, tuache kuzomea tukifanya hiyo tutakuwa tumejijengea heshima,” alisema Mama Anne.
Kwa upande wake mmoja wa mtoa mada katika semina hiyo, kuhusu haki za wanawake, utu, hali ya maisha na mgawanyo wa rasilimali, Ussu Mallya, ambaye pia ni wanaharakati wa masuala ya wanawake aliwataka wajumbe hao ,wanawake kutetea saula la Usawa wa Kijinsia liingizwe katika Rasimu ya Katiba likiwa ni
moja ya Tunu za Taifa.
Mtoa mada mwingine ambaye pia mjumbe Bunge hilo na ni Makamu Mwenyekiti wa TWPG, Suzan Lyimo alisema ni vema wanawake hao kupigania asiliamia 50 inakuwepo ili kuhakikisha masuala yote yanayohusu wakina mama yakuwemo, mfano kwenye nafasi za ubunge, ajira na ngazi zingine za maamuzi.
Suzan alisema hayo wakati akitoa mada kuhusu Uwakilishi wa wanawake, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mada nyingine iliyotolewa katika semina hiyo ni masuala ya miradhi na ndoa iliyotolewa na Victoria Mandari kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) ambaye aliwataka wajumbe hao kutoendeleza mambo ya mila na desturi ambayo yanamkandamiza mwanamke.
Katika semina hiyo, baadhi ya wanawake hao walipendekeza masuala ya haki ya elimu kwa wanawake, haki za uzazi salama, haki ya kumiliki mali, haki ya ulinzi kwa wanawake na watoto, haki ya mtoto wa nje ya ndoa, umri wa mtoto kuolewa kuwa ni miaka 18 kuingia katika rasimu hiyo.
No comments:
Post a Comment