Uwanja wa Jamhuri Dodoma ukiwa umejaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mcheze wa ligi ya mkoa hatua ya sita bora kati ya CDA na Sheli, kuvunjika katika dakika ya 54.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Mkoa wa Dodoma (DOREFA), Nassor Kipenzi akifurahia jambo pamoja na wajumbe wa kamati ya mashindano ya ligi ya kutafuta bingwa wa mkoa wakiwa katika uwanja wa jamhuri baada ya pambano kati ya CDA na Sheli kuvunja kutokana na Mvua kubwa kunyesha na kujaza maji.
Kocha wa Timu ya CDA, Juma Masugu akitoa maelekezo kwa wacheji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika ulioikutanisha timu yake na Sheli hata hivyo mchezo huo ulivunjika kutokana na mvua kubwa kunyesha wakati ukiendelea.
Timu ya Sheli ikitoka uwanjani wakati wa mapumziko huku ikiwa haijapata bao kama wenzao CDA kwenye uwanja wa Jamhuri kabla ya kuvunjwa na Mwamuzi Dominick Nyamsana dakika ya 54 kutokana na mvua kubwa zilizonyesha leo. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
Na John Banda, Dodoma
MVUA kubwa zilizoanza kunyesha dakika ya 2 kipindi cha pili cha mchezo wa ligi ya kutafuta bingwa wa mkoa wa Dodoma hatua ya sita bora kati ya CDA na Chinangali (Sheli) zalisababisha mchezo huo kuvunjika baada ya maji kuja uwanjani.
Mchezo huo ulioanza kwa timu hizo kuonekana kukamiana huku kukiwa na kosakosa za hapa na pale kutokana na kushamburiana kwa zamu mashabulizi ya kushtukiza ambapo mpaka mpambano huo ukivunjwa hakukua na timu iliyouona mlango wa mwenzake.
Mwamuzi wa mchezo huo Dominick Nyamsana alilazimika kupuliza kipyenga cha kuashiria kuuvuja mchezo huo Dakika 54 baada ya kuona mvua hizo zinaendelea kunyesha huku wachezaji wa timu zote mbili kushindwa kuuona mpira kutokana na ukungu uliosababisha wachezaji kuanguka hovyo.
Mjumbe wa kamati ya mashindano hayo Mrisho Somba alisema mchezo huo utarudiwa kwa dakika zilizobaki baada ya kamati hiyo kukutana na kupanga siku ambayo wataona kuna upenyo wa kufanya hivyo kutokana na ratiba inayoendelea.
Hata hivyo kumezuka wasiwasi kutoka kwa mashabiki wa mpira wa miguu mkoani hapa ambao wanadai kutokana na Chama cha mpira nchini TFF kuviagiza vyama vya mikoa kikiwemo Dorefa kutuma jina la Bingwa wa mkoa March 30 yaani jumapili hii kuna uwezekano wa ligi hiyo kutoisha na bingwa anweza kuwa si halali.
Mwenyekiti wa Dorefa Nassol Kipenzi alilifafanua hilo kwa kuwataka mashabiki kutokuwa na wasiwasi kwani tayali wameshaiomba TFF kuwaongezea muda mpaka Apr 9. 2014 kutokana na ligi hiyo kuchelewa kuanza kulikosababishwa na maadhimisho ya siku ya maji yaliyofanyikia katika uwanja huo wa Jamhuri.
No comments:
Post a Comment