TANGAZO


Saturday, March 29, 2014

Matukio mbalimbali katika picha kisiwani Pemba


MWENYEKITI wa mafunzo ya haki za binaadamu, kwa waandishi wa habari kisiwani Pemba, Ali Abass Omar, akifunga mafunzo hayo, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, kulia ni Mratibu wa kituo hicho Fatma Khamis Hemed, na katikati ni mtoa mada Asha Ali.
KUMEKUA kukijitokeza tabia mbaya ya wafugaji, kufunga mifugo kwenye maeneo ya skuli mbali mbali, ambapo mpiga picha wetu, alishuhudi dume la Ng’ombe katika skuli ya msingi ya Madungu mjini Chakechake,  likiwa linajipatia mlo kama liko malishoni.
MKUU wa Kamisheni ya Utalii Pemba, Suleiman Amour (mwenye kofia), akimtembeza mshindi wa droo ya kutembelea vivutio vya utalii Pemba, Agnes Barbra Tayari, wakiwa katika hoteli ya Misali nje kidogo ya mji wa Chake-chake, nyuma ni afisa habari kamisheni ya Utalii Zanzibar nd: Amour Mtumwa Ali.
Mwenyekiti wa wanajumuia ya wananchi wa Kengeja waishio Dar-es Salaam, Khalifa Mohamed Sultan (kulia), akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Kengeja, Mohamed Hamad, mashine ya fotokopi pamoja na vifaa vyengine kwa ajili ya skuli hiyo, vilivyotolewa na jumuia hiyo, vyenye thamani ya shilingi milion 4.9. (Picha zote na Haji Nassor, Pemba)

No comments:

Post a Comment