TANGAZO


Wednesday, March 12, 2014

Kituo kipya cha luninga cha TV1 Tanzania chazinduliwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha runinga TV1 Tanzania Bw. Marcus Adolfsson(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni mtangaziji wa habari wa kituo hicho Bw. Meshack Nzowa na Agness Sikaonga.
Msimamizi wa Kipindi cha "The One Show" Bi. Jokate Mwegelo akielezea namna kipindi hicho kitakavyosaidia jamii kupata burudani na fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wageni waalikwa. Kipindi hiki ni moja ya vipindi vitakavyokuwa vikirusha hewani na TV1 inayopatikana katika kisimbuzi cha Startimes kupitia channel namba 103.na kurushwa hewani kuanzia siku ya Jumatatu mpaka Alhamisi. Kulia ni mtangazaji mwenza wa kipindi hicho Bw. Ezden Jumanne na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa  TV1 Tanzania Bw. Marcus Adolfsson.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa  TV1 Tanzania, Bw. Marcus Adolfsson pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TVI akifuatilia kipindi cha  tamthilia ya Siri ya Mtungi ambayo inarushwa hewani na Kituo hicho,tukio hili limefanyika leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho
Mmoja wa waandishi wa habari wa TV Mlimani ambaye jina lake halikufahamika akiwa ameshikana mkono na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TV1 Tanzania, Bw. Marcus Aldolfsson baada ya kukabidhiwa kisimbusi cha Startimes kutokana na kushinda mchezo wa bahati nasibu ulioendeshwa wakati wa uzinduzi wa kituo hicho,jumla ya visimbuzi vitano (5) vilizawadi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa kituo cha runinga cha TV1 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benjamin Sawe - WHVUM)

No comments:

Post a Comment