TANGAZO


Tuesday, March 11, 2014

Bunge Maalum la Katiba lapitisha Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kulia), akizungumza jambo na mjumbe mwenzake, Brigedia Hassan Ngwilizi, wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti wa Kamati ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Profesa Costa Mahalu, akiwasilisha Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, katika kikao cha kujadili na kuipitisha, ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, wakati wa kikao hicho leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Muhagama, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba,katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, akichangia hoja hiyo, wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Panya Ali Abdallah, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, wakati wa kupitisha risimu hiyo, katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka kundi la watu wenye ulemavu, Frederick Msigala, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, wakati wa kupitisha risimu hiyo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, Vuai Ali Vuai, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka taasisi za Dini, Sheikh Mussa Kundecha, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akichangia hoja hiyo, wakati wa kikao kupitisha rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba leo.
Mmoja wa Kamati ya Rasimu ya Kanuni za Bunge la Katiba, Ismail Jussa Ladhu, akielezea kuhusu ufanikishaji wa rasimu hiyo pamoja na kutoa shukurani kwa wajumbe wote wa Bunge Maalum katika kufanikisha risimu hiyo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka taasisi za Dini, Askofu Amos Muhagati, akichangia hoja ya Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, akimlalamikia Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kwa kile alichodai kumnyima nafasi ya kuchangia hoja hiyo, wakati wa kikao kupitisha rasimu hiyo ya bunge hilo.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, akiendesha kikao hicho cha kujadili na kupitisha  rasimu hiyo, ya bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge kuhusu kile alichokuwa akikilalamikia kuwa ni kunyimwa nafasi ya kuchangia na Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho wakati wa kikao cha kupitisha rasimu za Kanuni za bunge hilo.


Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma.
WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba wameunga mkono azimio la kutunga na kupitisha kanuni za bunge Maalum la Katiba.

Wakiongea kwa nyakati tofauti ndani ya ukumbi wa bunge baadhi ya wajumbe waliopata nafasi waliwataka wajumbe wengine kuunga mkono na kupitisha azimio hilo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Aidha wajumbe hao waliwapongeza wajumbe walio katika kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni itakayotumika kuongoza bunge hilo kwa kazi waliyoifanya tangu kuanza kwa semina ya marekebisho ya kanuni hizo.

Pia wajumbe walimpongeza mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Bw. Pandu Ameir Kificho kwa kuongoza bunge hilo la uandaaji wa kanuni kwa umakini na busara.

Naye mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Bw. Pandu Ameir Kificho aliwataka wajumbe wenye nia ya kugombea uenyekiti wa Bunge hilo kwenda kuchukua fomu za maombi za nafasi hiyo katika ofisi za katibu wa bunge.

Kuhusu suala la Makamu mwenyekiti wa Bunge hilo Bw. Kificho alisema kwamba nafasi hiyo itajazwa pale mwenyekiti atakapopatikana kwani matakwa ya sheria ya bunge hilo yanataka nafasi hizo kuwa na wawakilishi toka pande zote mbili za Tanzania.

“Tunasubiri kumpata mwenyekiti kwanza kabla ya makamu mwenyekiti kwani sheria inasema iwapo mwenyekiti atatoka Tanzania bara basi makamu wake atatoka Zanzibar na vilevile kama mwenyekiti atatoka Zanzibar basi makamu wake atatoka Tanzania bara.” Alisema Kificho.

Mpaka jioni ya leo wajumbe 4 (nne) wameshachukua fomu hizo wakiwamo Samwel Sitta, Theresia Huviza, John Lifa Chipaka na Hashim Rungwe.

No comments:

Post a Comment