Mahakama nchini India imewapata na hatia watu watatu waliombaka mtawa wa kikatoliki wakati wa ghasia za kupinga dini ya kikristo katika jimbo la Orissa mwaka 2008
Mmoja wa waliotuhumiwa alipatikana na hatia ya ubakaji huku wengine wawili wakipatikana na hatia ya kumtomasatomasa mtawa huyo.Mashitaka iliyowakabili watuhumiwa wengine sita, ilitupiliwa mbali ktokana na kukosa ushahidi.
Mtawa huyo alibakwa na genge la wahindi siku moja baada ya ghasia kati ya watu wa jamii ya Hindu na wakristo.
Ghasia zilianza baada ya kiongozi wa dini ya Hindu kupigwa risasi na kufariki.
Magenge ya watu yalishambulia kanisa, meneo ya kuomba, nyumba na shule zinazosimamiwa na wakatoliki.
Zaidi ya watu 30 waliuawa na maelfu kuachwa bila makao kutokana na vurugu hizo.
Wanaume hao watatu watahukumiwa baadaye mwezi huu
No comments:
Post a Comment