TANGAZO


Wednesday, February 5, 2014

Waziri Fenella azindua program ya mafunzo ya mchezo wa Chess

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akihutubia wadau wa mchezo wa Chess alipokuwa mgeni rasmi katka chakula cha usiku kilichoandaliwa maususi kwa ajili ya kuzindua mpango wa kufundisho mchezo huo mashuleni. Hafla hiyo imefanyika jana  katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Bingwa wa zamani wa Duni wa mchezo huo GM. Garry Kasparov, Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania Geofrey Mwanyika (Mwenye tai).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akicheza Chess  na aliyekuwa bingwa wa Dunia wa mchezo huo GM. Garry Kasparov (kushoto) jana jijini Dar es Salaam kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa kufundisha mchezo huo mashuleni,  kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Chess Tanzania Vinay Choudary.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo Leonard Thadeo (mwenye tai nyekundu) kiwa na baadhi ya wadau wa mchezo wa ches wakifuatilia uzinduzi wa mpango huo wa kupeleka mafunzo ya mchezo wa chess katika shule hapa nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Dioniz Malinzi (kushoto) akisalimiana na Bingwa wa zamani wa mchezo wa Chess duniani GM. Garry Kasparov mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa kufundisha mchezo wa Chess mashuleni hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari)

No comments:

Post a Comment