TANGAZO


Wednesday, February 5, 2014

Gavana awaomba radhi wanawake Kenya

 


Gavana William Kabogo katika kongamano la magavana nchini Kenya
Mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya amewaomba radhi wanawake kwa matamshi yake wiki jana kuwa wanawake ambao hawajaolewa hawapaswi kushikilia nyadhifa za kisiasa.
Gavana wa kaunti ya Kiambu nje kidogo ya Nairobi, William Kabogo, amesema kuwa ikiwa wanawake wana umri wa miaka 35 na bado hawajaolewa basi wao sio timamu.
 
Aliongeza kuwa ikiwa hawana familia yao wenyewe basi wanawezaje kushughulikia maswala ya kitaifa na ya uongozi?
Matamshi ya Kabogo, yalimlenga mwanamke mmoja mbunge ambaye hana mume bali ana mtoto (Alice Ng'ang'a), ambaye alipinga pendekezo la gavana Kabogo la kuwatoza watu kodi mpya.
Msemaji wa shirika la maendeleo ya wanawake, (Rukia Subow) amemtuhumu Gavana huyo kwa ubaguzi na kuongeza kuwa uongozi ni akili ya mtu wala sio nguo anazovaa.
Kabogo alijibizana hadharani na Alice Ng'ang'a wiki jana kuhusu mapendekezo yake kama Gavana wa jimbo la Kiambu ya kuanza kuwatoza kodi wananchi kwa mambo fulani kwa lengo la kukusanya fedha za kuendesha miradi ya jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment