TANGAZO

Friday, February 14, 2014

Waendesha Bodaboda watakiwa kuondoka maeneo ya UDOM

Mmoja wa viongozi wa waendesha Bodaboda wanatoa huduma ya usafiri ndani na nje ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),  akiwagawia funguo za pikipiki zao, baada ya jana kutotoa huduma hiyo kwa zaidi ya saa 7, wakijadili nini cha kufanya baada ya kutakiwa kutopakilia abiria katika kituo hicho, kilichopo chuo cha Elimu ndani ya UDOM, Dodoma. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
Madereva wa Bodaboda wakiwa wamekusanyika pamoja, wakijadiliana jambo wakati wakifikiri nini cha kufanya baada ya kuona askari walinzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kuwafukuza na kuwataka kutopakilia abiria katika kituo hicho, kilichopo katika majengo ya Mchepuo wa Elimu.
Waendesha pikipiki za kusafirishia abiria maarufu kama Bodaboda wakiwa wameziegesha  katika kituo cha Daladala cha maktaba ya ualimu kilichopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDO). Madereva hao wamelalamikia kunyanyaswa na walinzi chuoni hapo kwa kukamatwa na kutishiwa kuvunjwa miguu bila sababu za kueleweka.

Moja ya Barabara zinazoingia katika jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), inavyoonekana. Barabara hizo zinalalamikiwa na uongozi wa chuo hicho, kutumiwa vibaya na waendesha bodaboda, ikiwemo mwendo kasi bila kufuata sharia.

No comments:

Post a Comment