Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abrahman Kinana (kulia), Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (wa pili kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto), wakiwa katika Mkutano wa siku moja wa Wabunge na Wawakilishi wa CCM katika ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Dodoma)
Baadhi ya Wabunge na Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakiwa katika mkutano wao, uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (kushoto), wakichukua maelezo wakati wa kikao cha siku moja cha Wabunge na Wawakilishi wa CCM katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (kulia), ambaye ni Mwenyekiti wa kikao cha Wabunge na Wawakiishi wa CCM alipokuwa akitoa taarifa za kikao hicho, mbale ya mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) katika ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Dodoma leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment