TANGAZO


Wednesday, January 29, 2014

Tahadhari ya njaa yatolewa Kenya

 

Mashirika mbali mbali yametoa tahadhari kuhusu uhaba wa chakula
Serikali ya Kenya imetoa tahadhari kuhusu tisho la nja kwa idadi kubwa ya watu kutokana na uhaba wa chakula.
Wizara ya kilimo imesema kuwa chakula kilichohifadhiwa kwa sasa kinaweza kudumu tu hadi mwezi Mei.
Wafanyabiashara wa sekta binafsi wametakiwa kuingilia kati na kununua chakula zaidi kutoka nje ili kuokoa hali.
Hii leo serikali imetoa tahadhari kuhusu uhaba wa chakula lakini wiki jana halmashauri ya serikali ya kukabiliana na ukame ilitoa tahadhari kwa serikali kuhusu tisho la ukame.
Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na ukame ni maeneo ya Mashariki ambako mvua haijanyesha kwa muda mrefu.
Mkuu wa halmashauri hiyo aliitaka serikali kuchukua hatua mwafaka ili kuzuia ukame na janga la njaa ambalo liliwahi kushuhudiwa nchini humo miaka kadhaa iliyopita.
Katika eneo la Turkana Kaskazini mwa Kenya ambako jamii za kuhamahama huishi, hali inasemekana kuwa mbaya zaidi.
Kuna ripoti za watu kukabiliwa na njaa pamoja na ukame. Mtoto mmoja aliripotiwa kufariki kutokana na njaa
Inaarifiwa watu kadhaaa wamelazwa hospitalini kutokana na utapia mlo huku familia moja ikilazimika hata kupika nyama ya Mbwa kutokana na ukosefu wa chakula.

No comments:

Post a Comment