TANGAZO


Saturday, January 4, 2014

Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein afungua kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia  kukifungua Kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe, Jimbo la Bumbwini ,Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Afya Juma Duni Haji. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kufungua Kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe, Jimbo la Bumbwini, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipatiwa maelezo kutoka kwa Daktari Dhamana, Abdulwahab  Mohamed, baada ya kukifungua Kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe, Jimbo la Bumbwini, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimuuliza suala Daktari wa huduma za Mama na  Mtoto, Halima Abdalla Saidi, wakati alipotembelea sehemu mbalimbali zinazotoa huduma katika kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya kukifungua leo, katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wasoma Utenzi kutoka Kiwengwa Kaskazini B, Ashura Abdalla na Pili Pandu, wakitoa burudani yao, wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe leo. Rais wa  Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alikuwa mgeni rasmi katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wananchi wa Kijiji cha Bumwini Kiongwe, wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza baada ya kukifungua Kituo cha Afya kijijini hapo leo,  katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,. 
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya katika vituo mbalimbali waliofika kujumuika na wafanyakazi wa kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe, Jimbo la Bumbwini, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao baada ya kukifungua kituo hicho leo,  katika  shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu wa Halmashauri wa Jimbo la Bumbwini, Hassan Ali Kombo, akisoma risala wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Afya cha Bumbwini Kiongwe leo, ambapo mgeni alikuwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika  shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa Bumbwini Kiongwe leo, mara baada ya kukifungua kituo cha Afya kijiji hapo,
katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk. Saleh Mohamed Jidawi na Waziri wa Afya, Juma Duni Haji.

No comments:

Post a Comment