Majeshi ya Lebanon yametangaza kuwa kamanda wa cheo cha juu wa
kundi la kigaidi la Al Qaeda katika nchi hiyo Majid Al - Majid amekufa akiwa
kizuizini.
Kamanda huyo ambaye ni raia wa Saudi Arabia, alikuwa ni kiongozi wa kundi la
Abdulha Azzam ambalo lina uhusinao na kundi la kigaidi la Al Qaeda, na ambalo
pia limekuwa likikiri kuendesha mashambulizi ya kigaidi na milipuko ya mabomu
kulenga maeneo yanayokaliwa na waumini wa madhehebu ya Shia katika siku za hivi
karibuni.Miongoni mwa mashambulizi waliyokiri kuhusika nayo ni shambulizi katika Ubalozi wa Iran nchini Lebanon.
Maafisa wa jeshi wanasema Bwana Al Majid amekufa kutokana na maradhi ya figo na kwamba hali yake ilikuwa imezorota.
Al Majid alikamatwa mwezi uliopita na alikuwa akishikiliwa katika kizuizi cha siri.
No comments:
Post a Comment