TANGAZO


Saturday, January 4, 2014

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. Willium Mgimwa wawasili nchini ukitokea Afrika Kusini

 
 
Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.
 

Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini
 
Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.
 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa. (Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)























Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa likishushwa kwenye machela na kupakiwa kwenye gari maalum la kubebea, Uwanja wa Ndege wa Zamani, dar es Salaam leo mara baada ya kuwasili ukitokea nchini Afrika Kusini, alikofia wakati akipatiwa matibabu. (Picha na Khamis Mussa)


Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa likishushwa nyumbani kwake, Mikocheni B leo, mara baada ya kuwasili ukitokea nchini Afrika Kusini, alikofia wakati akipatiwa matibabu.
Waombolezaji wakishusha jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa, wakati mwili huo ulipowasili nyumbani kwake, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam leo ukitokea Afrika Kusini alikofia wakati akipatiwa matibabu.




Baadhi ya wafiwa wakiwa katika misa maalum ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa mara baada ya kuwasili nyumbani kwake, Mikocheni B, Dar es Salaam leo. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
 
 
 
 
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa, Leonard Maliva, akiendesha misa ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa, wakati mwili huo, ulipowasili nyumbani kwake, Mikocheni Dar es Salaam leo, ukitokea Afrika Kusini, alikofia wakati akipatiwa matibabu. 
 
 
Mke wa marehemu, Dk. Mgimwa, Jane Mgimwa (wa pili kushoto), akiwa na waombolezaji pamoja na wanafamilia hiyo, nyumbani kwa marehemu leo.  

Baadhi ya viongozi, Mawaziri pamoja na wageni mbalimbali wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa marehemu, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Mikocheni B leo.  
Baadhi ya viongozi na wageni mbalimbali wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa marehemu, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Mikocheni B leo.  
 
 

Waombolezaji wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa marehemu Dk. William Mgimwa Mikocheni B leo. 

Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa marehemu Dk. Mgimwa Mikocheni B leo.
 
 

No comments:

Post a Comment