TANGAZO


Thursday, January 30, 2014

Rais Jakaya Kikwete, awaapisha Waziri na Manaibu, Ikulu jijini Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu waziri, waliokuwa wakiapishwa, Ikulu Dar es Salaam leo. (Picha zote na OMR)
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, katika hafla ya kuwaapisha Waziri na Manaibu, iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dk. Binilith Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dk. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri pamoja na Manaibu mawaziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wale wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Eng. Dk. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu mawaziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.

No comments:

Post a Comment