Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mjini, Mwangi Rajabu Kundya, akimnadi mgombea nafasi ya uwakilishi wa chama hicho, Jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, zilizofanyika Mbweni, Wilaya ya Magharibi Unguja jana. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo, Zanzibar)
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mahmoud Thabit Kombo, akiwahutubia wananchi waliofika katika kampeni zake, Mbweni Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Na Miza Kona – Maelezo Zanzibar 30/01/2014
"CHAMA Cha Mapindunzi (CCM) ni chama chenye kuleta maendeleo ambacho kinapinga ubaguzi na kuwatetea wananchi haki zao za msingi,"
Hayo yameelezwa jana huko Mbweni na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini, Mwangi Rajab Kundya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki.
Hayo yameelezwa jana huko Mbweni na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini, Mwangi Rajab Kundya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki.
Amesema kuwa kuna baadhi ya vyama Vya upinzani vinachochea kuleta ubaguzi nchini kwa kisingizio cha kutaka Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili kinyume na matakwa yao.
Aidha, amesema kuwa Zanzibar imeshapata mamlaka yake tangu baada ya Mapinduzi na kuundwa kwa chama cha Afro Shirazi Party (ASP), ambapo tayari ina viongozi kamili na sifa zake zote za kupata maamlaka hayo.
“Mamlaka kamili tayari yamepatikana tangu ilipoundwa ASP hivyo wanataka mamlaka gani tena”, aliuliza Kundya.
Katibu huyo ameeleza kuwa Zanzibar itaendelea kudumisha Muungano ambao unatetea wazanzibar na kuwaletea maendeleo ambayo wananchi wananufaika na matunda yake.
Amefahamisha kuwa CCM sio chama chenye kuleta ubaguzi kwa wananchi kwani kiko makini katiika kuwaletea maendeleo ya nchi.
Amesema CCM ina viongozi makini ambao ni wataalam wa uongozi hawayumbishwi na watu wasiopenda maendeleo ya nchi.
“Kiongozi wa watu lazima ajitie katika makundi ya watu ili aweze kujua shida zao kwa lengo la kutatua matatizo ya watu wao lakini wapinzani hawana utaala huo”, alifahamisha bwana Kundya.
Aidha Katibu huyo amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi wa CCM kwani ndiye atakaeweza kusimamia Muungano, kupigania haki ya wanzibari na maendeleo kwa jumla.
Naye mgombea Uwakilishi wa chama hicho Mahmoud Thabit Kombo ameahidi kuimarisha matawi ya CCM kwa kinamama na jumuiya za wazazi pamoja na kuwaimarisha na kuwashajihisha vijana katika mambo ya ajira.
No comments:
Post a Comment