Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimweleza Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Beatha Swai (kushoto) Mipango na mikakati mbalimbali ya wizara katika kuhakikisha wanawaendeleza vijana na kumtaka Katibu Tawala huyo kuendeela kuratibu shughuli za kimaendeleo kwa vijana.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Beatha Swai Akimweleza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mipango mbalimbali ya kuwaendeleza vijana kimaendeleo ikiwamo kuanzisha chombo cha kusimamia maendeleo kwa vijana cha Pwani Youth Centre of Excellence(PYCE) wakati wa ziara ya Kuangalia utekelezaji wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa na vijana katika Mkoa wa Pwani leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi.Beatha Swai wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kutoka katika mkoa wa Pwani wakati wa ziara kutembelea Miradi mbalimbali inayotekelezwa na vijana katika Mkoa wa Pwani leo, katika Ofisi ya katibu Tawala Mkoani Pwani.(Picha zote na Hassan Silayo - MAELEZO)
No comments:
Post a Comment