Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakisikiliza michango iliyokuwa ikiwasilishwa na wajumbe wa bodi hiyo katika kikao chake hicho jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, akichangia mada wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara baada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki jijini leo.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtevu akichangia wakati wa kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, akichangia katika kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, Dar es Salaam leo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda, akichangia katika kikao hicho cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, Dar es Salaam leo
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua leo asubuhi jijini Dar es Salaan. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo, kutoka Sumatra, akichangia mada katika kikao cha bodi hiyo, leo jijini.
Mbune wa Kawe, Halima Mdee, akichangia kwenye kikao hico cha Bodi ya Barabara jijini leo.
Mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo, akichangia mada katika kikao hicho, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akikikiendesha kikao cha Bodi ya Barabara, mara baada ya kukifungua leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mbunge wa ,Kinondoni, Idd Azzan na kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkoa ya Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akifafanua jambo, wakati akikiongoza kikao hicho, mara baada ya kukifungua leo asubuhi jijini Dar es Salaan. Kushoto ni Katibu wa Bodi, Theresia Mmbando.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakimsikiza Mwenyekiti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Sadiki, wakati alipokuwa akifafanua jambo.
HOTUBA YA UFUNGUZI WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA YA MKOA
WA DAR ES SALAAM TAREHE 07/01/2014
Mhe.
Idi Azzan (Mb) - Makamu Mwenyekiti wa Bodi
ya
Barabara, Mkoa wa
Dar es
Salaam
Ndg.
Theresia Mmbando – Katibu wa Bodi ya Barabara
Mkoa
Waheshimiwa
Wakuu wa Wilaya,
Waheshimiwa
Wabunge
Waheshimiwa
Wastahiki Mameya,
Wakurugenzi
wa Mamlaka za Serikali zote za Mitaa, Mkoani kwetu,
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ‘DART Agency’,
Wajumbe
wa Bodi ya Barabara,
Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Itifaki
imezingatiwa.
Asalaam
Aleikum,
Awali ya yote tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha
kuumaliza mwaka 2013 kwa salama na kutujalia kuingia mwaka 2014 kwa salama.
Niwatakie nyote mliohudhuria kikao hiki heri na fanaka katika mwaka mpya wa 2014.
Naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika kikao
hiki cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wetu.
Hiki ni kikao cha kwanza cha Bodi hii katika mwaka huu wa fedha
(2013/2014).
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwenu nyote kwa
ushirikiano mnaoendelea kutoa katika kusimamia maendeleo katika Mkoa wetu wa
Dar es Salaam. Mafanikio tunayopata
yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wenu katika kufuatilia ujenzi wa
miundombinu ya barabara za Mkoa wa Dar es Salaam. Naomba tuendelee na ushirikiano huo ili
tuendeleze Mkoa wetu kioo cha maendeleo ya nchi yetu.
Ndugu Wajumbe,
Agenda kuu ya kikao hiki ni kupata taarifa za utekelezaji
wa mipango na bajeti ya matengenezo ya barabara ya robo kwa kwanza ya mwaka huu
wa fedha 2013/2014.
Tunaishukuru Serikali kwa kututengea katika Bajeti ya
mwaka huu wa (2013/2014) fedha za barabara kwa Mkoa wa Dar es Salaam jumla ya
shilingi 79,411,306,680.00. Kiasi
hiki ni pamoja na fedha zilizotolewa kwa Meneja wa TANROADS Mkoa pamoja na
Halmashauri zote kwa mchanganuo ufuatao:-
1.
Kutoka kwenye Mfuko wa Barabara (Roads
Funds).
TANROADS - Shs. 56,203,520,000/=
Ilala - Shs.
1,964,380,000/=
Kinondoni -
“ 5,528,410,000/=
Temeke - “ 1,313,880,000/=
Jumla
Tsh. – “ 65,010,190,000/=
2. Kutoka vyanzo vya Halmashauri (Own
Source)
Jiji
la Dar es Salaam - Shs. 50,000,000/=
Ilala - “ 2,517,240,000/=
Kinondoni
- “ 5,385,000,000/=
Temeke - “ 3,043,241,680/=
Jumla Tsh. - “ 10,995,481,680/=
3.
Kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mfuko wa Maendeleo/Ruzuku.
Jiji la Dar es Salaam - Shs. 200,000,000/=
Ilala - “ 1,678,500,000/=
Kinondoni - “ 300,000,000/=
Temeke - “ 1,227,135,000/=
Jumla Tsh. - “ 3,405,635,000/=
Jumla Kuu Shs.
79,411,306,680/=
Hata hivyo kiasi hiki cha fedha ni kidogo kulingana na
mahitaji ya Mkoa. Pamoja na hayo kama
fedha hizi zikitumika na kusimamiwa vizuri mafanikio yanaweza kuonekana.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA
MATENGENEO YA BARABARA KWA (JULAI –
SEPTEMBA 2013).
Robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha ilianza
tarehe 1/7/2013
na kuishia tarehe 30/09/2013. Hali halisi ya utekelezaji hadi robo ya
kwanza inaisha Mamlaka za
Serikali za Mitaa na Wakala wa Barabara (TANROADS)
walikuwa kwenye mchakato wa manunuzi. Hivyo kazi nyingi
zilizofanyika ni zile za miradi ya viporo (roll-over)
vya mwaka uliotangulia wa 2012/13.
Kipindi hiki ni cha mvua hivyo pamoja na
jitihada
tunazofanya za kufanyia matengenezo
barabara, mashimo mapya nayo yanajitokeza katika barabara zote za changarawe na
za lami. Mashimo yote ni kero ila
ukikutana na shimo katika lami linakuwa ni kero zaidi na hatari kwa mwenye gari
na watumiaji wengine wote wanajitahidi kulikwepa shimo hilo. Hivyo basi,
kipindi kama hiki cha mvua Wahandisi wajipange zaidi kutumia ‘cold mix’ kuziba mashimo kwani kwa
taarifa niliyonayo ‘material’ hiyo haiathiriwi na maji hata wakati wa kuiweka.
Mkoa wetu umekuwa ukikumbwa na mafuriko kutokana na Jiografia
iliyopo na shughuli zingine za kibinadamu, tujipange kuchukua hatua za
kujihadhari na mafuriko ili tuwaepushe wananchi kukumbwa na mafuriko, kwa mfano
wakazi wa Buguruni Kisiwani, hivi karibuni walikumbwa na mafuriko sababu moja
wapo ni ujenzi holela na nyingine ni watu kujenga na kuzuia njia/mkondo wa
maji. Tabia ya kuwaacha watu wanajenga kama hakuna taratibu na sheria, tufike
mahali tuseme basi. Sheria za kudhibiti ujenzi katika mito na Bahari zipo
lakini nashangaa kwa nini hazisimamiwi ipasavyo na Mamlaka za Serikali za
Mitaa.
Nimepata taarifa ya kuanza ujenzi wa mfereji wa Bonde la
Mpunga, hii ni hatua nzuri. Hivyo nawataka wanao usimamia mradi huo TANROADS, Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni mshirikiane na Mkoa kuhakikisha mradi huo unafanyika
kwa wakati na kwa ubora ya hali ya juu.
Bado tatizo la usimamizi dhaifu ni kubwa jambo linalopelekea Mkandarasi
kutekeleza kwa kiwango cha ujenzi duni na hivyo miundombinu husika kuharibika
hata kabla ya kipindi cha matazamio.
Ndugu Wajumbe,
Taifa letu lina mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa
’Big Results Now’ kifupi BRN. katika mkakati huu sekta za kipaumbele zina
malengo waliyojiwekea, chonde nawaomba Wajumbe wa bodi hii tuwe imara hakutakuwa na msalie mtume. Kazi
lazima ifanyike,
Naamini ‘tukiamua tunaweza’, kwani mandhari
ya Jiji letu wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hali ya Jiji ilibadilika kabisa,
nawapongeza wote waliofanikisha ziara ile kubwa na kuipa sifa nchi yetu. Hivyo basi msimamo uwe ni ule ule katika
kuhakikisha malengo tuliyojiwekea katika BRN Kimkoa yanafikiwa kwa asilimia
mia. Kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo, tuache kufanya kazi kwa mazoea. Hili
litafanikiwa tukiwa wabunifu zaidi, makini zaidi na kuongeza usimamizi katika
kazi zetu za kila siku.
Aidha tupange mipango yetu tukizingatia
namna tutakavyo ondokana na msongamano katika Jiji letu ambayo ni changamoto
kubwa
Ndugu Wajumbe nawaomba mchangie kwa
ukamilifu mawazo na ushauri juu ya uboreshaji wa matengenezo ya miundombinu ya
barabara katika Jiji letu ili tuondokane na matatizo yaliyopo. Kabla ya kikao
hiki tulipata wasaa wa kukagua kazi zilizofanyika na zinazoendelea
kutekelezwa. Kila kikundi kitapata wasaa
wa kueleza yale waliyoyaona na kukosoa, kutoa ushauri kwa uwazi ili tuweze
kupata uthamani wa fedha (value for money) katika kazi za barabara
zinazofanyika.
Kwa hayo machache naomba kusema kwamba kikao
cha Bodi ya Barabara Mkoa kimefunguliwa rasmi.
ASANTENI SANA
No comments:
Post a Comment