TANGAZO


Tuesday, January 7, 2014

Matatani kwa kumfananisha Rais na Kiazi

 


Rais Michael Sata
Kiongozi mmoja wa upinzani nchini Zambia, amekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kumchafulia jina Rais wa nchi hiyo Michael Sata baada ya kumfananisha na Viazi
Frank Bwalya anadaiwa kumtaja Rais Michael Sata kama "chumbu mushololwa" kupitia kwa Redio siku ya Jumatatu.

 
Katika lugha ya Bemba, tamko hilo lina maanisha viazi vitamu ambavyo humegeka vinapopindwa , maana ya ndani ikiwa mtu ambaye hasikilizi ushauri wa wengine.
Bwana Bwalya anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.
Aidha Bwalya ni kasisi wa zamani na mfuasi wa zamani wa Rais Sata, ingawa sasa anaongoza chama cha muungano wa vyama vya upinzani (Alliance for a Better Zambia (ABZ).
Naibu waziri wa mambo ya ndani, Stephen Kampyongo alisema kwamba, bwana Bwalya alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia sifa Rais Sata.
''Rais Sata ni yule yule aliyekuwa anasikika kwenye vyombo vya habari habari akiwachafulia sifa marais wa zamani, Banda na Mwanawasa na hakuna aliyemkamata,'' alisema katibu mkuu wa chama cha ABZ Eric Chanda.
Viongozi wa upinzani wametaka Bwana Bwalya aachiliwe wakisema kuwa yeye ni mwanasiasa asiyemuogopa mtu.
Waliongeza kuwa matamshi ya Bwalya, "chumbu mushololwa" hayakuwa matusi.
Mnamo mwezi Sepetamba mwaka jana Nevers Mumba mwanasiasa mwingine wa upinzani, alihojiwa na polisi kwa kusema Rais Sata ni muongo.

No comments:

Post a Comment