Watu 30 wameuawa katika kijiji kimoja eneo la kati mwa Nigeria
katika jimbo la Plateu ambako kunaishi watu wa dini mbali mbali.
Kijiji hicho kiko katika eneo ambalo limekuwa likikumbwa na mzozo wa muda
mrefu wa kikabila.Washambuliaji wanaoaaminika kutoka jamii ya Fulani pia waliiba mifugo.
Msemaji wa kijeshi katika eneo hilo alithibitisha mauaji hayo lakini akasema kuwa ni mapema mno kuelezea idadi kamili ya watu waliouawa, ingawa uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa.
Maelfu ya watu wameuawa katika kipindi cha miaka mitatu katika mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya makabila hasimu katika mkoa wa kusini wenye wakristo na kaskazini wanakoishi waisilamu.
Vurugu katika eneo la Kati mwa Nigeria huchochewa na mizozo ya ardhi kati ya jamii za wahamiaji mfano kutoka jamii ya Fulani na wakulima mfano watu wa jamii ya Berom ambao ni wakristo.
Idadi hiyo ya watu thelathini waliouawa inajumisha watoto na wanawake
Maelfu ya watu wameuawa katika mizozo kama hiyo tangu mwaka 2010 lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa serikali haijachukua hatua za kuridhisha kukomesha mizozo hiyo.
No comments:
Post a Comment