TANGAZO


Friday, January 3, 2014

Mahakama Kuu yaahirisha kutoa uamuzi kesi ya Ombi la zuio la Kamati ya Chadema kumjadili Zitto Kabwe hadi Januari 6, mwaka huu itakapotoa uamuzi wake


Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (kulia), akifurahi wakati akipongezwa na mmoja wa wafuasi wa chama hicho, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, kuahirisha kesi ya ombi la zuio lililofunguliwa na mwanachama wa wa chama hicho, Zitto Kabwe dhidi ya Kamati Kuu ya chama, kumjadili hadi mahakama hiyo, itakapotoa uamuzi wake, Januari 06 mwaka huu. (Picha zote na Hamisi Mussa)
Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, akiwa amezungukwa na wafuasi wa chama hicho, baada ya Mahakama Kuu, kuahirisha kesi inayohusu ombi la zuio la kujadiliwa mwanachama Zitto Kabwe katika Baraza Kuu la chama hicho, ambapo sasa hukumu yake, itatolewa Januari 06, mwaka huu.
Askari wa Jeshi la Polisi, wakiwazuiya mashabiki wa pande mbili hizo, zinazopigana katika mgogoro huo, nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam leo. 
Askari wa Jeshi la Polisi, wakiwazuiya wafuasi hao, waliokuwa na mabango nje ya Mahakama Kuu baada ya Mahakama kuaghirisha uamuzi wa suala hilo leo. 
Wafuasi wa pande zinazopingana katika mgogoro huo, wakiwa na mabango mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 06, mwaka huu.
Askari wa Jeshi la Polisi walikiwatoa wafuasi wa Chama hicho pamoja na wale wa Zitto Kabwe.
Askari Polisi wakiweka ulinzi mkali nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam leo.
Wafuasi wa pande hizo, wakionesha mabango yao dhidi ya wenzao katika mgogoro huo.
Hali ilikuwa hivi kwenye Mahakam hiyo, jijini leo.
Wakili wa Zitto Kabwe Albert Msando akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania akiwa katika ulinzi mkali wa jeshi la Polisi huku wafuasi hao, waliokuwa  wakidhaniwa kuwa ni wafuasi wa chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakionesha mabango yao.
Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando akitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania akiwa katika ulinzi mkali wa jeshi la Polisi huku wafuasi hao, waliokuwa  wakidhaniwa kuwa ni wafuasi wa chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakionesha mabango yao.
Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando akiwapungia wafuasi wa chama hicho, wakati aktoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, baada ya kuahirishwa kwa kesi yake yake dhidi ya Kamati Kuu ya Chadema.
Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando akiwpungia mashabiki wa Chadema, wakati akitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando akiondoka Mahakam Kuu ya Mahakama Kuu ya Tanzania akiwa katika ulinzi mkali wa jeshi la Polisi' 

Mawakili wa Zitto Kabwe, wakiondoka mahakamani hapo baada ya kesi waliyoifungua dhidi uongozi wa Chama hicho jijini leo.

No comments:

Post a Comment