TANGAZO


Thursday, January 2, 2014

Jaji Warioba: Muungano wa Serikali tatu hauna gharama


 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto)  kikabidhi nakala za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mkuuwa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena (katikati) wakati wa mkutano baina yaTume hiyo na Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF), uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Januari 2, 2014. Anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto), akikabidhi nakala za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga wakati wa mkutano baina yaTume hiyo na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar esa Salaam leo, Alhamisi Januari 2, 2014.
Mwenyekiti waTume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (wa pili kulia akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa mkutano baina yake ya Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Januari 2. 2014. Wengine Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga, Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Makamu Mwenye kiti wa Tume, JajiMkuumstaafuAugstino Ramadhani. (Picha zote na Tume ya Katiba)

Na Mwandishi wetu

TUME ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, imesisitiza kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali tatu hauna gharama kubwa kama ambavyo inaelezwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa na badala yake gharama za uendeshaji zitapungua.

Imesema Muungano wa Serikali tatu utapunguza gharama hususan zinazotumika katika vikao vya kutatua kero na matatizo mbalimbali aliyomo kwenye Muungano wa Serikali mbili.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari Dar es Salaam leo katika mkutano uliohudhuriwa pia na wajumbe wa tume hiyo, alisema lengo ni kuondoa matatizo yaliyopo sasa kwenye Muungano.

Alisema Serikali tatu ndiyo tiba sahihi ya kuondoa kero mbalimbali zilizoko kwenye Muungano.

Jaji Warioba alisema lengo ni kuondoa matatizo ya Muungano, ambapo wao kama tume wamezingatia wananchi wanataka nini na namna ya kuyaondoa ili Muungano uendelee kudumu na si kuendelea na manung'uniko yaliyopo.

"Tukiwa na Serikali mbili na wakati kero za Muungano zipo, gharama bado zitakuwa kubwa, kwani fedha nyingi zitakuwa zikitumika katika kusuluhishana.

"Serikali tatu haitakuwa na gharama kubwa kwani idadi ya mawaziri na manaibu mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitazidi kumi na tano.

"Kimsingi ni kwamba gharama zitakuwa katika utawala hivyo sisi tume tunaamini gharama si tatizo kuwa na Muungano wa Serikali tatu. Watu wanasema Serikali tatu ni gharama lakini kwenye kuongeza mikoa hawaoni kuwa ni gharama," alisema Jaji Warioba.

Jaji Warioba akiendelea kuzungumza alisema kuwa waliyoyajumuisha katika Rasimu ya Katiba Mpya ambayo imekabidhiwa kwa Rais Jakaya  Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein mwanzoni mwa wiki hii kuwa hayakuwa mawazo yao bali ni ya wananchi.

Ambapo aliwataka Watanzania kutowahusisha wajumbe wa tume hiyo na makundi mbalimbali na kwamba wao wamefanya kazi ya wananchi kile ambacho wanakitaka na si vinginevyo.

"Tulipoteuliwa na Rais kuingia katika tume tulikuwa na imani, itikadi na misimamo tofauti, lakini tukakutana kwa lengo la kuwasikiliza wananchi na si itikadi zetu. Msimamo wetu tume ni kulinda maslahi ya wananchi na si chama chochote cha siasa au kundi fulani.

"Tusihusishwe na makundi bali mawazo ya wananchi. Sisi tumefanya kama Watanzania na tumewasikiliza wananchi baada ya kutoa sababu zao za msingi. Tuache mambo ya makundi," alisisitiza.

Pia aliwashangaa watu wanaobeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imemgeuka Mwalimu Julias Nyerere kuhusu muundo wa muungano.

Alisema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando kama watu wanaodai tume imemgeuka Baba wa Taifa na kueleza kuwa hata

yeye alikuwa analazimika kufanya marekebisho pindi anapoona kuna haja ya kufanya hivyo.

"Watu wanatulaumu wanasema eti tumemgeuka Mwalimu, hivi wanafikiri Mwalimu angekuwa na mawazo mgando tu siku zote?

Mwalimu alikuwa 'champion' wa vyama vingi baada ya kuona wananchi wanataka iwe hivyo," alisema.

Jaji Warioba pia alimmwagia sifa Rais Jakaya Kikwete na kuelezea kuwa ana nia ya dhati ipatikane Katiba Mpya na kwamba wao hawana

wasiwasi naye.

No comments:

Post a Comment