TANGAZO


Sunday, December 22, 2013

UN yasihi Sudan Kusini kuacha vita

 

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka vita dhidi ya raia nchini Sudan Kusini visitishwe, akisema ana wasiwasi mkubwa juu ya mapigano hayo yanayozidi.
Ametoa wito kwa Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar kutafuta suluhu ya kisiasa.
Wafanyakazi wageni katika visima vya mafuta wanaokimbia ghasia wamelezea jinsi wenzao raia wa Sudan Kusini walivokatwa shingo na vichwa vayo kubumundwa kwa mawe.
Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 60,00 wamekimbia makwao tangu mapigano kuanza juma lilopita.
Awali rais Obama aliwaonya viongozi wa Sudan Kusini kwamba juhudi zozote za kunyakuwa madaraka kwa nguvu zitapelekea Marekani na ulimwengu kuacha kuisaidia nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment