TANGAZO


Thursday, December 19, 2013

Rais wa Zanzibar Dk. Shein afungua kongamano la utafiti na ubunifu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania, Dk. Hassan Mshinda, wakati alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, lililofanyika leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Alex Maharindo wa Kampuni ya BR-Solution, ambayo inashughulika na utoaji wa Taarifa kwa watumiaji wa simu za mikononi, wakati alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, lililofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akipata maelezo kutoka kwa David Mung’ong’o, wa Blackmark-Poultry Expo Tanzania, Kituo kinachoshughulikia Kuku (ndege wanaofungwa), Ushauri, Maonesho ya wadau kama wafugaji, watengenezaji vyakula vya mifugo, watoa huduma, wanaouza dawa, vifaa, watotoleshaji vifaranga, wakati alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, lililofanyika leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akipata maelezo yanayohusu Mfumo wa kuhifadhi taarifa za Hospitali (HOSPITAL MANAGEMENT SYSTEM), kutoka kwa Editha Dismas Lyimo, wakati  alipotembelea  maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, lililofanyika leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Shaali Makame Ame (wa pili kushoto), Mtaalam  katika Maabara ya Afya ya Jamii Pemba (PUBLIC HEALTH LABORATORY_IVO DE CARNERI), kwenye maonesho katika Kongamano la Utafiti na  Ubunifu, lililofanyika leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akiangalia mashine ya ubunifu wa Umeme wa kufua kutumia (upepo hewa), ambayo imebuniwa na Ali Mahmoud Ali (kushoto), wakati maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, lililofanyika leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Baadhi ya wadau mbali mbali walioshiriki katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akitoa hutuba yake wakati alipolifungua leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Baadhi ya wadau mbali mbali walioshiriki katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akitoa hutuba yake wakati alipolifungua leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Profesa Idrisa A. Rai, alipokuwa akitoa salamu zake wakati wa Kongamano la Utafiti na Ubunifu, lililofanyika leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, alipokuwa  akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali  Mohamed Shein, kulifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akitoa hutuba yake wakati alipolifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort. Wa kwanza kulia ni Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA), Profesa Idrisa A. Rai, kushoto ni Dk. Hassan Mshinda, Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia  Tanzania, akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa hutuba yake, wakati alipolifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu leo, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort. Kulia ni Makamo Mkuu wa Chuo cha Taifa (SUZA), Profesa Idrisa A. Rai, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed.

Na Said Ameir, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kuwaendeleza na kuwaenzi watafiti watakaovumbua na kugundua mambo yenye faida kwa taifa na kwamba itaweka utaratibu maalum wa hadhi na heshima zinazostahiki kwa watafiti hao.
Sambamba na ahadi hiyo Serikali pia imesema itahakikisha fedha za bajeti za shughuli za utafiti zinaongezwa hatua kwa hatua ili mabadiliko kwenye mambo ya utafiti yaonekane waziwazi wazi.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati akifungua kongamano la siku moja la Utafiti na Ubunifu lililoandaliwa kwa pamoja na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar-SUZA, Chuo cha Sayansi ya Afya Zanzibar na Tume ya Sayansi na Tekinolojia Tanzania- COSTECH.
“Tutahakikisha kwamba watafiti wanaovumbua na kugundua mambo yenye faida kwa nchi yetu, tunawaendeleza na kuwatunza ipasavyo. Hizi ndizo ahadi zangu kwenu na nyinyi tekelezeni wajibu wenu” Dk. Shein aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo lililofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort iliyopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Hata hivyo alikiri kuwa Zanzibar kama zilivyo nchi nyingine barani Afrika inakabiliwa na changamoto kubwa ya ufinyu wa bajeti katika kugharimia shughuli za utafiti lakini akasema suala la gharama katika utafiti haliwezi kukwepeka kama nchi inataka kupiga hatua kimaendeleo kama zilivyofanya nchi nyingine duniani.
Akionyesha dhamira ya Serikali  anayoingoza kuhusu utafiti alibainisha kuwa kwa mwaka 2013 fedha zilizotengwa kwa shughuli hizo katika bajeti ya kawaida ni asilimia 0.041 sawa na asilimia 0.011 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na kiwango kilichotengwa huko nyuma kabla ya mwaka 2010 ambacho kilikuwa asilimia 0.0016 kwa bajeti ya kawaida sawa na asilimia 0.00055 ya Pato la Taifa.
Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein alisisitiza kuharakisha kuweka mpango maalum wa kitaifa utaokaoainisha vipaumbele vya Utafiti kwa mujibu wa mahitaji ya utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar Awamu ya Pili-MKUZA II pamoja na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020.
“Ziko wizara zina zimejipangia vipaumbele vyao vya utafiti lakini hatuna hakika kama  vipaumbele hivyo vinakwenda sambamba na vipaumbele vya taifa hivyo ni lazima tuunde mpango maalum utakaoanisha vipaumbele vyetu lengo likiwa kufikia malengo ya utekelezaji wa mipango yetu hiyo ya maendeleo”alisisitiza Dk. Shein.
Aliwataka watafiti nchini kujenga ushirikiano miongoni mwao wakiwa kama timu za kitafiti na ushirikiano baina ya taasisi zao katika kufanya tafiti zitakazowezesha kutoa majibu ya matatizo yanayowakabili wananchi.
“Ushirikiano wa aina hiyo ni muhimu kwa watafiti ili kujijengea uwezo na kuongeza uwezo wa kufanya tafiti zitakazokuwa na manufaa kwa taifa” alibainisha Dk. Shein.
Aliwahimiza watafiti na taasisi husika kutoa taarifa za kitafiti na matokeo ya tafiti walizozifanya na kusimamia matumizi yake ili kubadili maisha ya wananchi na kusukuma mbele maendeleo ya taifa.
Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein aliwapa changamoto wataalamu wa utafiti nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kuinua hali ya utoaji huduma za jamii kwa watafiti hao kufanya tafiti mbalimbali zitakazotoa mapendekezo muafaka ya kuimarisha huduma hizo.
“Tunahitaji michango na ushauri wenu nyinyi wataalamu na watafiti itakayotuwezesha kuwa na mbinu, mipango na sera bora zitakazotuwezesha kufikia malengo haya kwa ufanisi”alieleza Dk. Shein na kusisitiza kuwa huu si wakati tena wa kufanya mambo kwa kubahatisha.
Atumia fursa hiyo kuipongeza COSTECH kwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba kufanikisha shughuli za utafiti Zanzibar na kuzihimiza Wizara na Taasisi za Serikali kuzitumia fursa za utafiti zilipo kupitia Taasisi hiyo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali akizungumza kumkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alisema Serikali imekuwa ikitumia vizuri fursa za utafiti zitolewazo na Tume ya Sayansi na Tekinolojia nchini-COSTECH na kutaja baadhi ya shughuli hizo ambazo Tume hiyo imekuwa ikifanya humu nchini kwa kushirikiana na Serikali.
Alisema kuwa hivi sasa COSTECH inadhamini masomo ya shahada za juu kwa wanafunzi 21 wa Zanzibar, inasaidia utafiti katika masuala ya kilimo na mifugo pamoja na kusaidia kuimarisha chuo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUZA Prosesa Idris Raia alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuweka utaratibu maalum wa kuvishirikisha vyuo vikuu na Taasisi za Utafiti katika upangaji wa vipaumbele vya utafiti katika Wizara na Taasisi za Serikali.
Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali  akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi     

No comments:

Post a Comment