Makundi ya kutea haki za Binaadam nchini Misri yamekosoa uamuzi
wa mamlaka kuhukumu kifungo cha miaka kumi na mmoja dhidi ya kundi Waandamanaji
wa kike kutoka chama cha kiislamu nchini humo.
Wanawake 21 na wasichana walikamatwa mwezi uliopita baada ya kutokea
maandamano mjini Alexandria yaliyokuwa yakimuunga mkono Kiongozi aliyeondolewa
madarakani, Mohamed Morsi , huku Familia moja ikidai binti wa familia hiyo
alikamatwa alipokuwa akipita eneo lenye maandamano akielekea shuleni.Walithibitishwa kuwa na makosa ya kutumia nguvu na hujuma, lakini washtakiwa walikana wakidai kuwa maandamano hayo yalikuwa ya amani.
Mwandishi wa BBC jijini Cairo amesema kuwa hukumu iliyotolewa imedaiwa kudhihirika kwa kuwepo kwa utawala wa mabavu nchini humo.
No comments:
Post a Comment