TANGAZO


Friday, November 29, 2013

Tanzania kunufaika na mradi wa mbogamboga mashuleni

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa hafla ya utambulisho wa Mradi wa Kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda shuleni leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mradi wa Kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda Shuleni Dk. Usha R. Palaniswamy.
Meneja Mradi wa kupeleka bustani za mbogamboga na matunda shuleni, Dk. Usha R. Palaniswamy akifafanua jambo wakati wa utambulisho wa Mradi huo, hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Paulina Mkonongo na Mratibu wa Mradi Tanzania, Bi. Joyce Sekimanga.
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi. Paulina Mkonongo akisisitiza jambo kwa watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (hawapo pichani), wakati wa hafla ya utambulisho wa Mradi wa kupeleka Bustani ya Mbogamboga na Matunda shuleni leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa mradi huo, Bi. Bi Joyce Sekimanga
Mmoja wa watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo akichangia mada baada ya kutambulishwa Mradi  wa kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - Maelezo)

Na Frank Shija
Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache Barani Afrika zitakazo nufaika na mradi wa
kupeleka bustani za mbogamboga na matunda shule.

Hayo yamebainika wakati wa hafla ya utambulisho wa mradi huu ilyofanyika leo jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu  huyo amesema kuwa ni fursa nzuri kwa Tanzania kufikiwa na mradi huu kwa kuwa utasaidi kuongeza hamasa ya kutumia mboga za majani na matunda miongoni mwa jamii.

Aidha Prof. Mchome ameongeza kuwa ni Serikali imepoke mradi huu na kuhadi kushirikiana na wadau wengi katika kuhakikisha mradi huu unaendelea.

" Tumepokea kwa faraja kubwa mradi wa kupeleka bustani za mbogamboga mashule, nami naamini kuwa wanafunzi wetu watafurahi sana kwani utawaongezea maarifa lakini pia ziada inaweza kuuzwa na kutatua matatizo yao" Alisema Prof. Mchome.

Prof. Mchome aliongeza kuw utekelezaji wa mradi huu
utashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Afya na Ustawi wa
jamii.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Kupeleka Bustani za Mbogamboga Shuleni Dkt. Usha R. Palaniswamy amesema kuwa kutokana na umuhi wa virutubisho vilivyopokatika mbog
za majani na matunda taasisi yake iliamua kusaidi kuhamasisha matumizi yake kadri iwezekanavyo.

Dkt. Usha aliongeza kuwa kwa kupeleka mradi huu katika ngazi ya shule za Sekondary kutaleta hamasa kubwa kwa jamii kwa kuwa vijana wengi wa Sekondary ndiyo hao hao wanategemewa na familia zao.

Aliongeza kuwa nifaraja kwake kuona Tanzania inakuwa nchi ya pili katika utekelezaji mradi huu bara Afrika, kwani richa ya Tanzania pia unatekelezwa Burkinafaso kwa sasa na umefanikiwa sana.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari Bi. Paulina Mkonongo , amesema kuwa anaishukuru  taasisi ya AVRDC ambao ndio walioleta mradi huu hapa nchi kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali kwa kutekeleza baadhi ya program ambazo
zilikuwa zimeanza muda murefu.

Bi. Mkonongo amesema kuwa mradi huu utaongeza kasi na kuleta hamasa kwa wanafunzi na wazazi kujijengea utamaduni wa kulima bustani itakayo wapa faida mara mbili kwa kuwa watapata mboga na  matunda wakati huohuo kujipatia kipato kama ziada.

Mradi wa kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda unatarajiwa kuanza mapema mwezi wa kwanza 2014,utatekelezwa katika jumla ya shule za Sekondari 30 mkoani Morogoro, na baadae utasamba nchi nzima baada ya kuonyesha mafanikio katika awamu hii ambayo itakamilika mwishoni mwa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment